Tarehe 14 mwezi Oktoba ni siku ya kumbukumbu ya miaka 24 tangu Baba wa Taifa alipoaga dunia. Lakini tarehe hii kwa mwaka 2023 nisiku ambayo Mkoa wa Manyara unapokea heshima kubwa ya kuadhimisha siku ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Na heshima ya Mkoa kufanya shughuli ya kilele cha mbio za Mwenge kwa mwaka 2023 ni heshima kubwa iliyopewa Mkoa wa Manyara.
Sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa uhuru Mkoani Manyara ni neema katika mambo mengi kwanza ni kupokea ugeni wa Mwenge wa uhuru. Ambao ni alama ya amani na umoja katika Taifa letu Mwenge wa huru utawasili Mkoa wa Manyara katika Wilaya ya kiteto tarehe 7 mwezi Oktoba niwazi kuwa Mwenge utapita katika wilaya za Mkoa wa Manyara na utafanya uzinduzi wa miradi mingi.
Katika makala hii tuna angalia jinsi ambavyo Mwenge wa uhuru ujio wake na kilele chake kufanyika Mkoa wa Manyara utaenda kuleta mabadiliko ambayo yataenda kugusa maisha ya wananchi wa Mkoa wa Manyara. Nakuongeza kasi ya uchumi kwa mtu mmoja mmoja nihakika kuwa Mkoa wa Manyara utapokea ugeni mkubwa ambao niwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani.
Miongoni mwa kitu kizuri ambacho Mwenge wa uhuru utaenda kuweka alama kwa wananchi wa Mkoa wa Manyara ni ujenzi wa uwanja wa kisasa wa kwaraa. Uwanja ambao ndipo zitafanyika sherehe za kilele cha mbio za Mwenge hii itakuwa ni alama kubwa ambayo wananchi wa Manyara na Halmashauri zake hawata weza kusahau kwa miaka mingi katika fikra zao.
Ni uwanja ambao hata mala baada ya sherehe za kilele cha mbio za Mwenge bado utaendelea kuwa kitega uchumi na chanzo cha kuingiza mapato Mkoa wa Manyara. Lakini kutakuwa na mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya michezo katika Mkoa wa Manyara huwenda Mkoa ukapata timu itakayokuwa ikiwakirisha Mkoa wa Manyara katika ligi kuu ya Tanzania.
Kilele cha Mwenge wa uhuru Mkoa wa Manyara ni fursa kwa vijana wa Mkoa wa Manyara kwanini ni fursa kwa vijana kuna namna mbii katika fursa hizo. Mosi ni fursa ya maonesho ya wiki ya vijana kitaifa ambayo yatafunguliwa na Waziri Mkuu Mh. Kasimu Majaliwa Majaliwa hii ni fursa kwa vijana wa Manyara kuonesha ubunifu wao shughuli zao kwa namna yake huu ni mwanzo wa vijana wa Manyara kuonesha vijana wengine kutoka mikoa tofauti uwezo wao na maarifa yao waliyonayo.
Wiki ya vijana itawapa wigo mpana vijana wa Mkoa wa Manyara na mikoa mingine inayotarajiwa kushiriki kwenye wiki hiyo, kufamiana nakubadilishana ujuzi wakimaarifa n.k. lakini kongamano la vijana ambalo linatarajiwa kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 150 litasaidia vijana kusema changamoto zao nakujadili mambo mengi yenye muktadha wakumfanya kijana kuwa mzalendo na mwenye mafanikioa ndani ya Taifa lake.
Fursa ya pili ni vijana wa Mkoa wa Manyara kujiinuwa kiuchumi au kuweza kubadirisha maisha yao kupitia kilele cha mbio za Mwenge 14 mwezi Oktoba 2023.
Niwazi kuwa huu ni ugeni mkubwa ambao Mkoa unaenda kuupokea boda boda watanufaika kwa usafirishaji wa watu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine migahawa itapata ongezeko la wateja kuliko iliyo kawaida wa miiki wa Hoteli kubwa wataongeza wigo wa watu.
Mkoa utaenda kuwa na mzunguko wa fedha ambao kimsingi unatokana na shughuli za kilele cha mbio za Mwenge wa uhuru.
Lakini Mwenge wa uhuru kupitia ujumbe wake wa mwaka 2023. ‘’TUNZA MAZINGIRA OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA VIUMBE HAI NA UCHUMI WA TAIFA’’ ujumbe huu unatukumbusha kulinda mazingira ilikuondokana na tatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi linayoweza kujitokeza.
Mwenge wa Uhuru unatutaka kila mtu awe barozi katika utunzaji wa mazingira ikiwa ni upandaji wa miti pia unatukumbusha kulinda misitu yetu. Mkoa wa Manyara una vivutio vingi vya utalii na mandhari yenye kuvutia ni jukumu la kila mwananchi kuendelea kuwa sehemu yakutunza uwoto wetu wa asiri ambao mungu ameubariki kupitia mbuga zetu Tarangire Manyara na milima mizuri inayo vutia katika Mkoa wa wetu.
‘’Karibu Mwenge wa uhuru, karibu Manyara Home of Tanzanite and Elephant’’
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.