Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara wakiongozwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi. Coleta Shayo leo tarehe 3/8/2018 walijitokeza kumpokea Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bw.Missaile Musa aliyeteuliwa siku ya Jumamosi na kuapishwa siku ya Jumatano tarehe 1/8/2018 katika ukumbi wa Kikwete Ikulu Jijini Dar es slaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt. John Pombe Magufuli.
Mapokezi hayo pia yalihudhuriwa na wawakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Babati, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mji Babati na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Babati.
Mara baada ya mapokezi hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara alifanya mazungumzo mafupi na Wakuu wa Idara na Vitengo na kuwataka kufanya kazi kwa bidii katika kuwatumikia wananchi wa Manyara na Tanzania kwa ujumla. (Kwa picha za matukio mbalimbali angalia sahemu ya kituo cha Habari kishanenda maktaba ya picha.
Imeandikwa na: Haji A.Msovu (Afisa Habari Mkoa wa Manyara)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.