Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bw.Missaile Musa leo Jumatano tarehe 26 Februari, 2020 ametiliana saini mkataba wa Baraza la wafanyakazi na Mwenyekiti wa Baraza hilo Tawi la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara Mhandisi Norbert Kyomushola.
Mkataba huo upo kama na agizo la Mheshimiwa Rais Na.1 la mwaka 1970 pamoja na sheria ya Majadiliano ya pamoja katika utumishi wa Umma Na 19 ya mwaka 2003 na kanuni zake,sheria ya ajira na mahusiano kazini Na 6 ya mwaka 2004 na kanuni zake, Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7 ya Mwaka 2004, pamoja na Majadiliano ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2003 (Public Service Negotiating Machinery Act ), makubaliano hayo ni Mkataba kamili wa ushirikishwaji wa wafanyakazi wa Sekretarieti ya Mkoa.
Akielezea Madhumuni ya Mkataba hu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Tawi hilo Mhandisi Norbert Kyomushola alisema kuwa “Kama Taasisi ya Umma Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara ni lazima iwe na Baraza la Wafanyakazi katika kuendesha shughuli zake ili kuwezesha kuimarisha mahusianao mazuri kati ya wafanyakazi na Sekretarieti na hivyo kuboresha utekelezaji wa mipango ya Sekretarieti”.
Mabaraza ya wafanyakazi yanaundwa kwa kufuata masharti haya mbalimbali ikiwemo Kutengeneza Mkataba wa Miundo ya Vikao na Kanuni za Baraza, kuandaa Mafunzo mbalimbaili pamoja na ya haki na wajibu wa Wafanyakazi yatabidi yatolewe na Viongozi wa TUGHE kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Watu wenye ulemavu,Kugharamia kutengeneza Mkataba na kuendesha Mafunzo hayo kwa Wafanyakazi na Wakufunzi ni juu ya Sekretarieti yenyewe pia uchaguzi halali wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi unatakiwa usimamiwe na Wizara ya Kazi na Ajira, Tume ya Ususruhishi na Uamuzi kitengo cha Elimu kazi kwa kushirikiana na viongozi wa TUGHE Mkoa.
Ili uundaji wa Baraza la Wafanyakazi na utekelezaji wa Mkataba uwe unatakiwa kukamilika si zaidi ya muda wa siku thelathini (30) toka Mkataba uliposajiliwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Watu wenye ulemavu Makao Makuu.
(Kwa picha mbalimbali angalia sehemu ya Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.