Ni kikao cha 5 cha maandalizi ya shughuliya kilele cha mbio za Mwenge katika Mkoa wa Manyara kilichoongozwa na Mh. Queen Sendiga pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Mh. Korolina Mthapula na kamati nzima ya ulinzi na usalama Mkoa wa Mayara 18.8.2023 katika ukimbi namba 83 ofisi za Mkuu wa Mkoa.
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa amepokea taarifa ya maendeleo ya miradi inayofanyika katika Halmashauri hasa miradi ambayo itakayozinduliwana na ukaguliwa na Mwenge wa uhuru. Hata hivyo taarifa zote kuhusu miradi inayoendelea katika Halmashauri hasa miradi itakayo kukaguliwa na Mwenge wa uhuru imeonyesha iko katika hali ambayo ni nzuri na yenye kuridhisha.
Kila Halmashauri imewashirisha taarifa yake mbele ya Mkuu wa Mkoa na vyombo vya ulinzi na usalama. Pia kamati zilizoundwa katika vikao vilivyopita nazo zimewasirisha taarifa za maendeleo katika kikao hicho ambapo kila kamati imeonyesha maendeleo ya maandalizi mazuri.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesisitiza juu ya uboreshaji wa miradi hiyo inayoendelea katika Halmashauri. Katika kikao hicho Mh. Queen Sendiga amemkabidhi taarifa ya maandalizi kwa ujumla Katibu wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara ambae pia alikuwa miongoni mwa wajumbe waliyo hudhuria katika kikao hicho.
katibu wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara amepongeza kwa maandalizi mazuri yanayofanywa na Halmashauri zote sanjari na hilo amemwambia Mkuu wa Mkoa kuwa chama cha mapinduzi kimeandaa vijana wapatao 400 ambapo kila Wilaya itatowa vijana 50 kwajili yakutoa hamasa kwa watu.
Pia ameeleza vijana hao watakaa kambi ya siku 3 kwaajili ya kufanya semina ya mafunzo ya itifaki ikiwa nikuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kilele cha mbio za Mwenge wa uhuru.
Mh. Queen Sendiga amesisitiza juu uwaandaaji wa nyaraka za miradi kuwa tayari ametaka nyaraka hizo zijumuishe na nyaraka za kimira ilikutambua mradi kama uko kwenye eneo la Serikali.
Ametoa rai kwa watendaji na wakurugenzi kukutana na wananchi nakusikiliza kero zao ilikutoweza kujitokeza kwa mambango ya kero za wananchi katika kilele cha mbio za Mwenge suala ambalo linaweza kuwa ni dosari kwa utendaji kazi kwa viongozi.
‘’Tunza mazingira okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa’’ ujmbe wa mbio za Mwenge mwaka 2023,
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.