Katibu Mkuu ofisi ya waziri Mkuu Profesa Jamal Adam Katundu na katibu tawala Mkoa wa Manyara Mh Karoline Mthapula.
Julai 20. 2023 amefanya kikao cha tathimini ya maandalizi ya kilele cha mbioa za mwenge wa uhuru. Ambapo itakuwa siku ya kuzimwa kwa mwenge wa uhuru kitaifa Mkoa wa Manyara umepewa heshima kubwa ya kuzimiwa kwa Mwenge Mkoa wa Manyara.
Lengo mahususi katika kikao hicho ikiwa nikushirikiana kwa pamoja ilikufanikisha maandalizi mazuri katika kuelekea siku hiyo muhimu, Aidha katibu Mkuu ame karibisha ubunifu katika maandalizi hayo ilikuweza kufanya kilele cha kuzimwa mwenge wa uhuru mwaka 2023 kuwe na utofauti na hasa ikizingatia kuwa Mkoa wa Manyara umepewa heshima hiyo kubwa kwa mwaka 2023.
Amewashukuru kwa maandalizi mazuri katika hatua za awali kwa kamati nzima ya Mkoa wa Manyara kwa jinsi wanavyo endelea na ufanisi wa maandalizi, Sambamba na hivyo amepokea taarifa ya jumla kutoka kwenye kamati ya Mkoa wa Manyara katika hatua zake zenye kulidhisha nakutoa muelekeo mzuri.
Mratibu wa mbio za Mwenge Mkoa wa Manyara Samweli Pastory akiwasilisha taarifa ya maandalizi ameeleza kuwa hadi sasa bajeti ya mwenge iko tayari ambayo ni Tsh 1,934,317,126, sambamba na hilo mratibu huyo wa mbio za mwenge Mkoa wa Manyara ameeleza kamati ya maandalizi imefanikiwa kuandaa sare ya Taifa katika mbio za mwenge kwa mwaka (2023).
Pia ameeleza juu ya maandalizi ya wiki ya vijana ambayo yamepangwa kufanyika uwanja wa Ccm Mkoa wa Manyara. Sambamba na hilo pia kamati ya Mkoa wa Manyara katika maadalizi yake imefanikiwa kufanya zoezi la upimaji Afya kwa wanafunzi wa alaiki, Pamoja na mratibu kuwasilisha taarifa lakini kila kamati imewasilisha taarifa yake mpaka ilipofikia katika maandalizi.
Kamati ya chakula Afya na vinywaji
Kamati hiyo imefanikiwa kuandaa watu wakutoa msaada wa dharuala katika upande wa afya wakishirikiana na madaktari wa Mkoa wa Manyara.
Ikiwa nikatika namna tatu tofauti namna ya kwanza ni madaktari kwajili ya watu wote ambapo kutakuwa na shirika la msalaba mwekundu kwajili ya huduma ya kwanza.
Lakini pia kamati imeendaa madaktari mahususi kwajili ya wageni maalumu ambao watakuwa wamealikwa, Madaktari kwajili ya kuhudumia vijana wa alaiki ilikuepusha suala la vijana hao kuanguka wakati wa shughuliza uwanjani zinapokuwa zikiendelea.
Kamati pia imeandaa usafi wa mazingira kwajili ya uwanja wa kwaraa ili kukinga na kulinda Afya za watu ambao wata hudhuria katika siku hiyo,
Aidha kamati hiyo itaanda chakula ambacho kitakuwa kwa makundi mablimbali na tayari maeneo yamekwisha tengwa na Mkoa kamati hiyo imewasilisha taarifa hiyo mbele ya jopo zima ambalo limeambatana na katibu Mkuu kutoka ofisi ya waziri Mkuu.
Kamati ya ratiba risala na miradi
Kamati imefanikiwa kuandaa vitambulisho kwa makundi mbalimbali ambayo yata hudhuria katika kilele hicho cha mbio za mwenge, pia imefanikiwa kufanya uwandaaji wa salamu kwa Mkuu wa Mkoa.
Kamati ya halaiki na hamasa
Kamati hii imefanikiwa kuandaa vijana wapatao 1200 wa Mkoa wa Manyara katika ushiriki wa shughuli mbalimbali hasa katika wiki ya vijana, imefanikiwa kuandaa mpango wa kuhamasisha upimaji wa Afya kwa wananchi wa Mkoa wa Manyara katika kuelekea kilele cha kuzima mwenge wa uhuru.
Kamati ya maonyesho ya wiki ya vijana
Maonyesho ya wiki ya vijana kamati imeandaa kwanzia tarehe 8 – 9 oktoba maonyesho ya wiki ya vijana, kamati imefanya utambuzi wa makundi ya vijana watakao andamana ikiwa matarajio ya kamati nikuwa na vijana 3000, Utambuzi wa vijana watakao husika na maonyesho (wajasiriamali).
uwandaaji wa mdahalo utakao husisha vijana zaidi ya 150 ikiwa nikujadili mambo yanayo wahusu vijana katika nyanja za kiuchumi na kijamii, ikiwemo mchango wa vijana katika shughuli za kiuchumi na kijamii. Sambamba na hayo pia kamati imefanya utambuzi wa miradi ya mkakati kwajili ya uzungukaji wa mwenge lakini pia uwandaaji wa bonanza la michezo ya jadi.
Aidha katibu Mkuu akiambatana na katibu tawala Mkoa wa Manyara na jopo la wataalamu kutoka ofisi ya waziri Mkuu, Ametembelea kanisa la Roho mtakatifu ambalo itafanyika Misa takatifu ya kumbukizi ya siku ya kifo cha Mwalimu Nyerere oktoba 14 ikiwa sehemu ya ukaguzi wa maandalizi kuelekea siku hiyo ambayo ndio kilele cha mbio za mwenge kitaifa.
Pia katibu Mkuu (profesa Jumal Adam katundu) ametembelea uwanja wa shule ya Babati day ambao utakuwa ukitumika kwajili ya mafunzo kwa vijana wa alaiki,
Ametembelea eneo la uwanja wa Ccm stendi ya zamani ambao utatumika kwa maonyesho ya wiki ya vijana pia amefanya ukaguzi wa uwanja wa kwaraa ambao utatumika kwa shughuli ya kuzima mwenge wa uhuru, Amefurahishwa na maandalizi mazuri yanayoendelea akizipongeza kamati zote na uongozi wa Mkoa wa Manyara kwa ujumla.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.