Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe Charles Makongoro Nyerere amewataka wananchi kujitokeza kuwaandikisha watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano kupata vyeti vya kuzaliwa.
Mhe Charles Makongoro Nyerere ametoa kauli hiyo katika kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano katika Mkoa wa Manyara.
Amesema Idadi ya watoto waliosajiliwa katika mkoa wa Manyara imeongezeka kutoka asilimia 6.3 na kufikia asilimia 80.2.
Naye Katibu Mkuu wizara ya katiba na Sheria Bi Mary Makondo amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa lengo la kuleta maboresho ya
mfumo wa usajili kupitia Mkakati wa Kitaifa wa Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu ambayo ni Vizazi, Vifo, Ndoa, Talaka na Watoto wa Kuasili.
Ameeleza kuwa Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri chini ya Miaka Mitano ni uthibitisho wa sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha watoto wanasajiliwa na kupata nyaraka ya awali na ya msingi ya utambulisho ambayo ni cheti cha kuzaliwa.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.