Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mtoto yalifikia kilele siku ya jumanne ya tarehe 7/8/2018 mkoani Manyara wilaya ya Babati katika kijiji cha Nakwa ambapo Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Babati Bw.Charles Mtabho alisema maadhimisho hayo yalilenga kukumbushana kuelemishana , kuahamasishana na kuepeana elimu juu ya unyoyeshaji .
Pia alisema “nimefurahishwa na kina mama wa kijiji hiki kuwa wameelimika na wameuthibitishia umma kuwa watoto wao wana afya njema na nawaomba kina mama hawa waendelee kunyoyesha mpaka watoto wao watakapofikisha miaka miwili”, pia alisema kuwa wao kama wahudumu wa afya wako mstari wa mbele kuhakikisha jamii inaiga mfano kutoka kwao sio kwa maneno tu bali pia kwa vitendo.
Aidha mgeni rasmi katika hafla hiyo Bw.Mabula katika hotuba yake ya maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji ililenga uhamasisha kwa kina mama kuwanyonyesha watoto wao katika miezi sita ya mwanzo kwani humpa mtoto asilimia 50 ya nguvu ambazo mtoto huitaji katika miezi sita ya mwanzo na asilimia 35 katika miezi sita hadi kumi na mbili na pia alisema unyoyeshaji hupunguza kupata saratani ya matiti na kizazi pia ni rafiki wa kiuchumi na humsaidia mtoto kupata virutubisho sahihi kwa ajili ya ukuaji wa akili na mwili.
Bw. Mabula aliwaahidi wananchi kutekeleza huduma mbalimbali kama ya usafiri ,uwepo wa takwimu za kijiji na wilaya na alifurahishwa na muamko wa wanawake waliopata elimu ya unyonyeshaji na jinsi ambavyo wakina mama hao wamejikita kujikwamua kiuchumi katika kilimo cha bustani na ufugaji wa wanyama wadogowadogo ambapo wanaingia katika siku elfu moja za unyonyeshaji.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “UNYOYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA NI MSINGI WA MAISHA”
(Kwa Picha mbalimbali za matukio ya wiki ya unyonyeshaji angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Imeandikwa na: Isabela Joseph (Mwanafunzi wa UDSM(SJMC)- Mafunzo kwa vitendo)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.