Wizara ya fedha na mipango tarehe 18. julai. 2023 imeendesha mafunzo mafupi kuhusu Dira ya maendeleo ya Taifa 2050 katika Mkoa wa Manyara.
Ambapo kaulimbiu ya mafunzo hayo ni ‘’shiriki katika kuijenga Tanzania uitakayo’’ mafunzo hayo yamefunguliwa na Mh Queen Sendiga Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Katika ufunguzi wa mafunzo hayo Mh Queen Sendiga amewaeleza washiriki katika mafunzo hayo lengo la mafunzo hayo nikupata uelewa wakutosha kuhusiana na dira ya maendeleo 2050, Aidha amewambia washiriki Dira hiyo inagusa maeneo yote katika Taifa hivyo kuna ulazima wa kila mwananchi kuwa na uwelewa huwo.
Amewaambia washiriki mafunzo hayo nimpango mahususi katika kuhamasisha watanzania wote na kuweka wepesi wakuweza kutumia mawazo ya kila mwananchi, Amewahakikishia wataalamu waliyoendesha mafunzo hayo kuwa uhamasishaji huwo kwa Mkoa wa Manyara utashuka hadi katika ngazi za wilaya na vitongoji.
Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa amewataka wakurugenzi katika Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara kupeleka uhamasishaji huwo katika ngazi za kata, ikiwa nikuwapatia taarifa za mafunzo hayo watendaji wa kata na wenye viti wa mitaaa ili kila mtanzania awe na uwelewa wakutosha kuhusu Dira ya maendeleo ya Taifa 2050.
Aidha mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mafunzo hayo (SoSthenes Kewe) kutoka wizara ya fedha na mipango ameeleza kuwa kwasasa inatumika Dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, Ambapo Dira hiyo ya 2025 ilikuwa nikuhakikisha Taifa linaingia katika uchumi wa kati ambao unachagizwa na kuboresha hali ya maisha kwa mtanzania kujenga utawala bora kujenga uchumi imara na shindani.
Mjumbe huyo ameeleza umuhimu wakuleta mafunzo hayo katika ngazi ya Mkoa ikiwa niutekelezaji wa Dira huku kiongozi mkuu wa Dira hiyo ya mwaka 2050 akiwa ni Mh Rais Samia Suluhu Hasani huku wenye dhamana wakiwa ni viongozi wa Mkoa.
Katika mafunzo hayo mjumbe huyo ametoa ufafanuzi katika Dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, Akionyesha mafanikio makubwa ikiwemo kupanda kwa pato la mwananchi. Kutoka USD(dora za kimarekani) 338 kwa mwaka 2020 hadi USD (dora za kimarekani) 1212 mwaka 2021 ambapo uchumi wa Taifa ulikuwa kwa wastani wa asilimia 6.
Aidha Dr Sarema mwenyekiti wa jopo la wataalamu hao kutoka wizara ya fedha na mipango katika maneno yake ya shukrani kabla ya Mkuu wa Mkoa kufunga mafunzo.
Amewashukuru washiriki katika mafunzo hayo huku akiwataka kila mmoja kuwa na wajibu wakutoa uhamasishaji huwo kwa Mkoa wa Manyara huku akisisitiza juu ya umuhimu wa watu wa Manyara kutoa maoni kuhusu Dira hiyo ya maendeleo kwa Taifa 2050.
Pia Dr Sarema amewaeleza washiriki kuwa mafunzo hayo nisehemu ya awamu ya kwanza katika utoaji wa maoni hivyo amewataka kila mmoja kujiandaa hasa katika taasisi za kiserikali.
Akionyesha umuhimu wa maoni amewataka watu wa Mkoa wa Manyara kutoa maoni yao bila ya kutoa maoni yao Mkoa wa Manyara hakutakuwa na mabadiriko katika nyanja mbalimbali kwenye mkoa.
‘’shiriki katika kujenga Tanzania uitakayo’’
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.