Julai 17. 2023 saa tano asubuhi jopo la wataalamu kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa wametoa mafunzo kuhusu mrejesho wa matokeo ya sense 2022.
Ambapo mgeni rasimi katika mafunzo hayo ni Spika wa Bunge staafu Kamisaa wa Sensa Mh Anna Makinda. mafunzo hayo yenye kaulimbiu ya ‘’Mipango jumuishi kwa maendeleo endelevu’’
Mh Anna Makinda ameeleza utofauti wa Sensa ya mwaka 2022 na Sensa silizopita nikatika kuhesabu vitu vyote ikiwemo majengo kaya na vitu mbalimbali ikilinganishwa na Sensa zilizopita zikijikita katika idadi ya watu pekee, Ameeleza kuwa Sensa ya mwaka 2022 imekuwa na uchakataji wa taarifa mpaka kwa makundi maalumu.
Amewataka washiriki katika mafunzo hayo mafupi kutumia fursa ya mafunzo hayo kwajili ya kwenda kuwezasha ufanikishaji wa uboreshaji wa huduma za kijamii.
Pia ameeleza ahadi za viongozi nilazima ziendane na Takwimu halisi ya watu lakini pia Kamisaa huyo wa Sensa amewataka washiriki katika mafunzo hayo ya muda mfupi kufikisha mafunzo hayo hadi kwenye ngazi za wilaya.
Ameeleza juu ya wajibu wa Serikali kubuni vyanzo vya ajira kutokana na ongezeko la watu hasa vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa, sambamba na hivyo amewataka vijana kutumia fursa zinazowazunguka kuweza kujiajiri wenyewe.
Lengo la mafunzo hayo ikiwa nikuweka uwiyano hasa katika miradi inayoanzishwa na Serikali katika Sekta ya Elimu na Afya, Ikiwa pia nikufanya urahisishaji wa shughuli za Serikali kwa ujumla ilikuweza kuendana na ongezeko la watu sambamba na kuongezeka kwa uelewa wa watu.
Katika mafunzo hayo katibu Tawala Mkoa wa Manyara Mh Karolina Mthapula amewaeleza washiriki kuwa Mkoa wa Manyara ulipata bahati ya kufanya majaribio ya Sensa mwaka 2021 – septemba, Ambapo Kamisaa wa Sensa ndiye aliye fanya shughuli hiyo , Ametoa shukrani zake za dhati kwakuweza kupata nafasi hiyo kwa malanyingine tena katika Mkoa wa Manyara.
Mwenyekiti wa mafunzo hayo Mh Queen Sendiga (Mkuu wa Mkoa wa Manyara) ametoa shukrani kwa ofisi ya Takwimu ya Taifa, pia amewataka watumishi wa Serikali waliyo hudhuria mafunzo hayo kuyaweka katika mipango yao ya kazi ilikuweza kufikisha huduma za kijamii kulingana na uhitaji wa idadi ya watu.
Kupitia mafunzo hayo mafupi imeonyesha Mkoa wa Manyara unaidadi ya watu Milioni moja na lakinane na tisini na mbili kwa Sensa ya mwaka 2022 ikiwa niongezeko kubwa la watu zaidi, Ambapo Sensa ya mwaka 2012 Mkoa wa Manyara ulikuwa na idadi ya watu laki tisa. Lakini Mkoa wa Manyara una Almashauri 5 na wilaya yenye watu wengi ni wilaya ya Babati yenye idadi ya watu 129,572,
Mkoa wa Manyara unaongezeko la watu kwa asilimia 32.4 ambapo Halmashauri ya Babati inaongezeko la watu Asilimia 37.8, Ambapo wilaya ya kiteto inaongezeko la asilimia 31.6, ikiwa ndio ongezeko la watu kwa asilimia chache kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara, Halmashauri ya wilaya ya Mbulu ina idadi ya asilimia 6.8 ikiongoza kwa idadi hiyo kwa upande wa wazee kwa Mkoa wa Manyara.
‘’mipango jumuishi kwa maendeleo endelevu’’
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.