Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amesema kuwa Wananchi wa Mkoa wa Manyara ndio wanufaika wakubwa wa maendeleo yaliyoletwa na serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani kwa kuwa serikali imeleta maendeleo katika sekta mbalimbali katika maeneo ya Afya,Maji,Kilimo,Barabara,Elimu,Maji n.k
Waziri Mkuu ameyasema hayo jana katika Mkutano wa hadhara uliofanytika katika Viwanjwa vya Kwaraa Mjini Babati alipokuwa katika ziara ya kuwanadi wagombea Ubunge na udiwani wa Mkoa wa Manyara.
“Wana Babati, wana Manyara nyie ndo sehemu ya wanufaika wakubwa wa mpango uliowekwa vizuri wa mpango wa ilani wa Chama Cha Mapinduzi na nyie ndo mtakaonufaika na mpango huu wa maendeleo kuanzia mwaka 2020 hadi 2025” Alisema Mhe. Majaliwa.
Mheshimiwa Waziri Mkuu hakuacha kuzungumziaa juu ya maombi ya wananchi wa Mbulu kuomba kuigawanya Halmashauri ya Mbulu kutokana na ukubwa wake na Serikali ilikubaliana na ushauri huo na kuamua kujenga Makao makuu wa Halmashauri na Jengo la Makao Makuu wilayani Mbulu ili kuweza kuwasogezea wananchi huduma.
Serikali imejenga Zahanati Zaidi ya 1195 Nchi nzima kwa kipindi cha miaka mitano na mkakati ni kila Kijiji kuwa na zahanati ili wananchi waweze kuhudumiwa huko walipo,Hospitali za wilaya katika Hospitali za Wilaya Halmashauri ya Wilaya ya Babati imepewa Shilingi Bilioni moja na nusu,kujenga hospitali za mikoa katika Mikoa mipya kumi na kuziboresha kutoa huduma,Hospitali za Kanda tatu zinajengwa ili wananchi wasipate tabu ya kwenda Muhimbili.
Pia amezungumzia kuhusu ujenzi wa kituo cha Afya cha Mutuka kumejengwa na vituo vya Nkaiti na Magugu vilivyotengewa shilingi milioni mia nne kila kituo katika Halmashauri ya Mji wa Babati na Halmashauri ya Wilaya ya Babati na kuleta Zaidi ya Milioni ishirini kila mwezi kwa ajili ya kununulia dawa,kuajiri madaktari kuanzia Hospitali za Mikoa,Wilaya,Vituo vya Afya na Zahanati.
Vilevile Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itakapoagiza Magari ya kubebea wagonjwa italeta magari mawili ya Wagonjwa kwa Halmashauri za Babati Mjini na Babati Vijijini.
Kwa upande wa sekta ya Elimu Mheshimiwa Waziri Mkuu amewataka Madiwani kuhakikisha wanasimamia fedha zinazoletwa na Serikali zinatumika ipasavyo ili kuepukana na michango kwa wazazi ikiwa ni Pamoja na kusimamia miundombinu ya shule zetu.
Akizungumzia ujenzi wa Barabara Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema Serikali ina mpango wa kuunganisha Barabara za lami kutoka Mkoa mpaka mkoa nchi nzia na baadae kujenga barabara za wilaya kwa wilaya.
“Tutajenga Barabara kwa kiwango cha lami kutoka Babati hadi Simanjiro na Barabara ya Karatu,Mbulu Hydom mpaka Simiyu” Alisema Mheshiwa Majaliwa.
“Pia Dongobeshi tumeshaanza ujenzi wa Barabara za lami na Babati Mjini tumetleta shilingi Bilioni 15.2 kwa ajili ya barabara za lami na barabara zenye urefu wa KM 8.1 za lami zimejengwa mjini Babati” Alisisitiza Mhe.Majaliwa.
Pamoja na kuelezea maendeleo yaliyoletwa na Serikali ya awano ya tano Mheshimiwa Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa pia amezindua kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Manyara kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28.
Viongozi mbalimbali wa serikali na Chama ni miongoni mwa waliofurika katika uzinduzi huo.
Waziri Mkuu aliwataka wagombea Udiwani na Ubunge kuhakikisha wanarudisha mashamba yote ya wawekezaji yasiyoendelezwa na kupewa wananchi waweze kulima na kujenga.
Mwaka 2020 Magufuli atapambana na wagombea urais wengine 14 huku Watanzania 29.2 milioni waliojisajili kupiga kura wakitarajiwa kushiriki zoezi hilo ikilinganishwa na 23 milioni waliojisajili mwaka 2015.
Chama cha Mapinduzi mkoa wa Manyara kina wagombea saba katika Majimbo ya Mbulu Mjini na Vijijini,Babati Mjini na Vijijini, Simanjiro, Hanang na Kiteto.
Mgombea Ubunge Jimbo la Babati mjini Paulina Gekul ambaye alichukua hatamu za uongozi 2015 akiwa Chama kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) anawania nafasi hiyo akitafuta muhula wa pili.
Jimbo la Mbulu, Wabunge waliomaliza muda wao Flatey Masay wa Mbulu Vijijini na Zakaria Isaay wa Mbulu Mjini wamerejea kwenye kinyang'anyiro.
Jimbo la Hanang anagombea Eng Samuel Hhayuma aliepishwa na Dr.Marry Nagu wakati Jimbo la Kiteto mgombea ni Wakili Edward Ole Lekaita na Simanjiro anagombea aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ambaye amepishwa na James Ole Millya.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.