Mkoa wa Manyara unaopatikana kaskazini mwa Tanzania una wilaya tano ambazo ni Babati,Simanjiro,Kiteto,Hanang na Mbulu. Ni Mkoa ambao unaongoza kuwa na madini ya aina mbalimbali hapa nchini.
Mkoa wa Manyara umebahatika kuwa na madini katika kila wilaya kiasi ambacho unaweza kusema hakuna mkoa wowote Tanzania ambao wilaya zake zote zina utajiri wa madini na hii ndo sababu tunaweza kujivunia na kuuita Mkoa wa Madini na kudhihirisha msemo wetu unaosema “Manyara the home of Minerals”
Akisoma taarifa ya Mkoa wa Manyara kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara yake Mkoani Manyara huko Mirerani Wilayani Simanjiro tarehe 14 /11/2018 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Alexander Mnyeti alionesha jinsi gani Mkoa wa Manyara una hazina kubwa sana ya madini nchini Tanzania.“Mh. Makamu wa Rais yaani kwa utajiri huu wa madini yaliyopo Manyara hata madini mengine hayajaanza kuchimbwa kwa hiyo tunawaombawawekezaji wa ndani na nje kuja Manyara kuwekeza katika sekta ya madini” Alisema Mh.Mnyeti.
Ili kuonesha jinsi gani Mkoa wa Manyara ni tajiri katika madini angalia jinsi kila wilaya ya Mkoa wa Manyara ilivyo na madini
Babati hunapatikana madini aina ya Emerald,Alexandrite,Almandite,Aventurine na Pozzzolana.
Almandite
Alexandrite
Pozzzolana
Aventurine
Emerald
Simanjiro kuna madini ya Tanzanite,Tsavorite,Toummaline,Rhodolite,Graphite,Grossulanite,Lolite,Amethst,Ruby na Limestone.
Tanzanite
Rhodolite
Grossulanite
Graphite
Tsavorite
Ruby
Mbulu pia kuna madini ya Pose Quartz,Gold (Dhahabu) na Pyrite
Pose Quartz
Pyrite
Gold (Dhahabu)
Madini aina ya Obsidian,Topaz na Salt(Chumvi) yanapatika katika wilaya ya Hanang.
Topaz
Obsidian
Salt(Chumvi)
Katika wilaya ya Kiteto unaweza kupata madini ya Ruby,Aquamarine na Moonstone
Aquamarine
Ruby
Moonstone
Upatikanaji wa madini hayo ndani ya Mkoa wa Manyara unaongeza kipato cha wananchi kwa kutoa ajiara za moja kwa moja kwani wamiliki wa viwanda wataajiri vijana kutoka mkoani Manyara kwa mfano kiwanda cha Madini ya Graphite kilichopo Mirerani katika wilaya ya Simanjiro kimeajiri wafanyakazi mia tano!! na pia kuna ajira zisizo za moja kwa moja kama mama lishe, wafanyabiashara mbalimbali N.K.
Hakika “Manyara the home of Minerals”
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.