Mkoa wa Manyara umekisia kutumia zaidi ya bilioni 198 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika mwaka wa fedha 2021/22.
Akizungumza katika kikao cha ushauri cha Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joseph Mkirikiti alisema kuwa kati ya fedha hizo zaidi ya bilioni 181 ni ruzuku kutoka serikali kuu,mapato ya ndani zaidi ya bilioni 16 na wanatarajia kutumia zaidi ya 129 kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi huku wakipanga kutumia zaidi ya biloni 42 katika miradi ya mendeleo na zaidi ya bilioni 9 zitatumika kwa matumizi mengineyo.
“Nazitaka halmashauri zote katika Mkoa wa Manyara kuhakikisha mnatumia vema fedha zilizotengwa ili ziweze kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wetu”alisema Mkirikiti.
Wakitoa maoni katika kikao hicho wajumbe mbalimbali walishauri miradi ya maendeleo kukamilika kwa wakati ili kupunguza adha kwa wananchi.
Jumla ya miradi mbalimbali 362 inatarajiwa kutekelezwa katika mkoa wa manyara ambapo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itatekeleza miradi 14, Halmashauri ya mji wa Babati miradi 39, Halmashauri ya wilaya ya Babati miradi 41, halmashauri ya wilaya ya Hanang miradi 99, halmashauri ya mji wa Mbulu miradi 29, halmashauri ya wilaya ya Mbulu miradi 68, halmashauri ya wilaya ya Kiteto miradi 29 na halmashauri ya wilaya ya Simanjiro miradi 43.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.