Jumuiya ya maridhiano ya amani imezinduliwa rasmi leo tarehe 4 Oktoba ,2018 katika Mkoa wa Manyara ambapo lengo la jumuiya hiyo iliundwa kwa maslahi ya Wananchi na serikali ili kuleta amani kwa taifa zima na lengo kuu la mkutano huo na jumuiya kwa ujumla ni kuona na kuhakikisha amani inadumishwa ili kuleta maendeleo.
Akitoa hotuba katika kikao hicho Katibu wa jumuiya ya maridhiano ya amani Tanzania Askofu Oswald Herman Mlay alisema kuwa “amani haiwezi kujengwa kwa vita,migogoro na hata mauaji hivyo ni jukumu letu kuhakikisha amani ya mkoa huu inalindwa pamoja na taifa zima lakini pia ni jukumu letu viongozi wa dini na Serikali kuhakikisha amani inakuwepo baina yetu kwani chombo hiki ni daraja kati ya Wananchi" alisistiza
Aidha katika ufunguzi huo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Alexander Mnyeti alisema “sisi kama serikali ya Mkoa tunawashukuru sana viongozi wa dini kwani wanafanya kazi kubwa ndani ya mkoa wetu kuhakikiasha amani inakuwepo na hatuna mashaka na tumeuona umuhimu na msingi wa jumuiya hii na tumeipokea kwa dhati na tuko tayari kutoa ushirikiano" Alisisitiza.
Hivyo tunawaomba viongozi wa dini kuzidi kutoa elimu za kidini na kimaadili na kukemea vitendo vya mauaji ya walemavu wa ngozi (albino),ndoa za utotoni na mimba za utotoni na migogoro ya ardhi ili amani izidi kutawala kwa ngazi ya mkoa hata taifa kwa ujumla.
(Kwa Picha mbalimbali angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Imeandikwa na Isabela Joseph (UDSM-Mafunzo kwa Vitendo)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.