Maonesho ya Nanenane mwaka 2018 Kanda ya Kaskazini yalifanyika Mkoani Arusha katika viwanja vya Themi kuanzia tarehe moja yamefungwa rasmi leo tarehe 8/8/2018 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi, Vijana,Ajira na Wenye ulemavu Mh.Jenista Mhagama.
Mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo Mheshimiwa Waziri akiongozana na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Mrisho Gambo alitembelea mabanda mbalimbali ya kilimo na mifugo na kujionea bidhaa zitokanazo na kilimo na mifugo.
Akiwakaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bwana Missaile Musa aliwashukuru waoneshaji waliojitokeza kuonesha bidhaa zao katika viwanja hivyo na kuwataka wawekezaji hasa katika sekta ya kilimo na ufugaji kuja katika mikoa ya Manyara,Arusha na Kilimanjaro kwani kuna maeneo mengi ya uwekezaji.
Akimkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira alimshukuru Mgeni rasmi kwa kukubali kwake kuhudhuria tena kuja kufunga maonesho hayo kwa mara ya pili mfululizo na kuwataka wananch kujifunza yale yote wanayoyaona kwenye viwanja hivyo na kuyapeleka kwenye Halmashauri zao,mashambani na kwenye makazi yao ili kuwaletea maendeleo.
Akihutubia wataalam,Wakulima,Wafugaji,Wavuvi,Wajasiriamali na Wananchi mbalimbali waliohudhuria aliwashukuru kwa kujitokeza kwao na kuwataka kuiuinga mkono Serikali katika juhudi za kuleta maendeleo kwa wananchi bila ubaguzi wa aina yoyote kwa kilimo,mifugo na uvuvi ni sekta ambazo zinachangia ajira kwa asilimia zaidi ya 65 kwa watu wote na pia inachangia uwepo wa chakula na shughuli mbalimbali za sekta ya kilimo, misitu na mifugo zimeongezeka kwa asilimia 3.6 mwaka 2017 kulinganiha na asilimia 2.9 kwa mwaka 2016. Pia alisema kuwa Sekta ya kilimo ilichangia pato la Taifa kwa asilimia 30.1 mwaka 2017 ukilinganisha na asilimia 29.2 kwa mwaka 2106.
“Ni lazima Serikali,na wadau kuipa sekta ya kilimo kipaumbele sekta ya kilimo” Mh.Waziri alisistiza.
Katika kuhakikisha Serikali inongeza tija tija kwa wafugaji serikali imezifuta tozo zilizokuwa kero kwa wafugaji, wakulima na wavuvi ili sekta sekta hiyo ilete tija kwa kwa Nchi.
Mhiushimiwa Waziri aliwataka wakulima,wafugaji na wavuvi kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu tano za kuboresha sekta hiyo.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni “Wekeza katika Kilimo,Ufugaji na Uvuvi kwa maendeleo ya Viwanda”
(Kwa Picha mbalimbali za matukio ya Nanenane angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Imeandikwa Na:Haji A.Msovu (Afisa Habari Mkoa wa Manyara)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.