Tarehe 8. 8. 2023 ni sikukuu ya ya wakulima inayofanyika kila mwaka. Sikukuu hiyo kwa mwaka 2023 imefanyika kikanda ikijumuisha mikoa ya Arusha Kilimanjaro pamoja na Mkoa wa Manyara mikoa ambayo inakamilisha ujumla wa mikoa ya ukanda wa kaskazini.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh Queen Sendiga amewaongoza maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Arusha katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima.
Kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima kwa mwaka 2023 kimefanyika kikanda katika Mkoa wa Arusha kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha.
Ambapo Mh Queen Sendiga akiwa ndiye mgeni rasimi watukio hilo kubwa, sambamba na hilo Mkuu huyo wa Mkoa wa Manyara ametembelea mabanda ya maonyesho pamoja na kuhutubia umma uliyojitokeza.
Amewataka wadau na wananchi kutumia fursa zilizopo katika kilimo cha umwagiliaji ilikukabiliana na mabadiriko ya tabia ya nchi. katika tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Manyara ametoa rai kwa wataalamu na maafisa wa kilimo kuyafikia makundi ya wanawake vijana na wananchi kwa ujumla ilikuwaongeza elimu na ufanisi katika shughuli za kilimo na ufugaji.
Aidha ameeleza kuwa Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya umwagiliaji kwenye ukanda wa mikoa ya kaskazini yenye thamani ya jumla ya Bilioni 47.64. vile vile ameeleza mpango wa Serikali kujenga visima 150 kwa kila Halmashauri ilikuleta mapinduzi katika Sekta ya umwagiliaji.
Pia Mh Queen Sendiga ameongeza siku mbili zaidi kwa maonyesho hayo kuendelea katika viwanja hivyo baada ya kuridhishwa na maonyesho kwa wakulima, wananchi na wanafunzi waliyojitokeza kujifunza kupitia maonyesho hayo.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.