Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Manyara Mh.Alexander Mnyeti amepokea ugeni wa Mawaziri Nane wa Serikali ya awamu ya tano Wilayani Simanjiro katika kijiji cha kimotorok leo ziara ambayo inalenga kutatua migogoro kati ya wananchi waishio katika vijiji vya orbokishu na wananchi wa kijiji cha kimotorok dhidi ya wahifadhi wa Pori tengefu la Mkungunero na hifadhi ya Tarangire.
Kamati hiyo imetokana na kamati iliyoundwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa chini ya Mwenyekiti Waziri wa Ardhi Mh. William Lukuvi na kuwateua Mawaziri wa Kisekta ikilenga kupata maoni, kujionea, kujiridhisha na kuandaa taarifa itakayomshauri Rais katika suala zima la kutatua Mgogoro huo kati ya wafugaji na wahifadhi wa wanyamapori katika maeneo hayo.
Akiongea katika ziara hiyo Mh. Lukuvi alinukuu kauli ya Rais aliyosema “Vijiji vyote vilivyo Ndani ya Hifadhi vibaki kama vilivyo”
Lukuvi alitia mkazo katika hili kwa kuwaeleza wahifadhi wasiwabughudhi wananchi kwani wanamkasirisha Rais. “wamasai hawakati miti wala hawali nyama pori, kwa sasa tumekuja kuwakumbusha tu mtambue nini Rais wetu anataka” alisema Lukuvi.
Wakizungumza mara baada ya mkutano huo wananchi wa Kijiji cha Kimotorok walifurahishwa sana na ujio huo wa Mawaziri katika eneo lao na kuwa na uhakika wa kuishi kwa amani bila bugudha yoyote.
(Kwa picha mbalimbali angalia sehemu ya Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Imeandikwa na:Haji A.Msovu
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.