Na Phabian Isaya
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amefanya ziara ya ukaguzi wa Zahanati ya Secheda iliyopo kata ya Secheda ambapo walipokea fedha za ujenzi wa Zahanati hiyo na ujenzi ulianza mwezi wanne 2023.Ujenzi huo mpaka sasa umefikia hatua yenye kuridhisha. Amefurahishwa na mwenendo wa mradi huo.
Aidha ameongeza kuwa Ujenzi wa Zahanati hiyo utawasaidia kata ya Secheda na vijiji vyake mradi huo ukikamilika na amewapongeza wananchi kwa kuchangia million 47 katika ujenzi huo hiyo ni hatua nzuri katika maendeleo.Amewataka kuendelea na moyo huo kujitolea kwa miradi mingine ya maendeleo itakaletwa katika kata hiyo.Pia amewapongeza wananchi wa Secheda kwa kushiriki kujenga madarasa manne kwa nguvu zao mwenyewe.
Vilevile Mhe. Queen Sendiga amefanya ukaguzi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Secheda iliyopo katika kata ya hiyo. Ambapo shule ya Sekondari Secheda ilipokea fedha kwaajili ya ujenzi tarehe 30/6/2022 kiasi cha cha fedha Sh Milioni 584 ambapo mradi ulianza 14/7/2023 wananchi pia wamechangia katika mradi huo wa ujenzi wa shule hiyo.
Sambamba na hilo Mhe.Queen Sendiga ametembelea eneo la Ushoroba (sehemu ya kupitia wanyama) iliyopo kata ya Nkaiti wilaya ya Babati Vijijini. Ambapo amewataka mamlaka husika katika hifadhi hizo kuweka mipaka ili kutoleta migogoro katika maeneo hayo ya hifadhi ya Tarangile na Manyara.
Pia Diwani wa Kata ya Nkaiti amewashukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na wataalam wake kwa kutembelea eneo hilo, ameanisha uwepo wa uvamizi wa tembo katika vijiji jirani katika eneo hilo la Ushoroba.Aidha Mkuu wa Mkoa amesisitiza juu ya ushirikiano ili kujua wavamizi na ambao sio wavamizi katika eneo hilo.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.