Na Phabian Isaya
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga leo terehe 16/9/2023 ametembelea kiwanda na Ofisi za kampuni ya Mati Super Brand zilizopo kata ya Bagala. Mhe. Queen Sendiga amepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. David Damian Mulokozi . Ameangalia jinsi shughuli za uzalishaji wa bidhaa za Mati Super Brand sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa wa Manyara ametembelea ofisi za vitengo mbalimbali ikiwemo kitengo cha ugavi na manunuzi pamoja na uhasibu.
Kampuni ya Mati Super Brand imeajiri watu 312 ambapo wenye ajira rasmi ni watu 124 Mkuu wa Mkoa wa Manyara amefurahishwa namna kampuni hiyo ilivyowaajiri watu wengi wa Mkoa wa Manyara, Pia amesisitiza kampuni hiyo kuongeza uzalishaji zaidi ilikuweza kutanuwa wigo wa uwekezaji zaidi.
Vilevile ameshukuru kwa uwekezaji mkubwa ambao kampuni hiyo imeufanya nakuajiri wazawa wengi kutoka Mkoa wa Manyara. Aidha amefurahishwa kuona kampuni ikimilikiwa na watanzania nakuweza kuleta mchango mkubwa katika mambo mengi ya kijamii na amewashukuru kwa mchango wao katika shughuli ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Ameeleza kuwa tarehe 10/10/2023 Mkoa wa Manyara utafanya uzinduzi wa jarida la uwekezaji katika Mkoa amewakaribisha wawekezaji kuwekeza katika Mkoa wa Manyara. Aidha ameeleza jinsi ambavyo Serikali imeweka mazingira rahisi na rafiki kwa wawekezaji ameahidi kutoa ushirikiano wakutosha na kampuni ya Mati Super Brand.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mati Super Brand ameshukuru kwa ujio wa Mkuu wa Mkoa katika Ofisi za kampuni hiyo ikiwa nikuonyesha Serikali ya Mkoa wa Manyara inatambua mchango wa kampuni hiyo. Ameahidi kutanuwa wigo zaidi ilikuongeza ajira katika kampuni hiyo afurahishwa na mazingira mazuri ya uwekezaji yanayowekwa na Serikali.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.