Na Phabian Isaya
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga akiwa katika ziara yake ameweka jiwe la msingi Shule ya mpya ya Awali na Msingi Queen Cuthbert Sendiga kata ya Maisaka Halmashauri ya Mji wa Babati. Ambapo shule hiyo ni mradi wa BOOST wa kuimarisha na kuboresha elimu ya Awali na Msingi hapa Mradi huu unatekelezwa nchini kwa muda miaka 5 hivyo kukamilika mwaka 2025/2026 na umelenga kunufaisha miundombinu ya elimu kwa madarasa ya Awali na Msingi.
Pia Mhe.Sendiga amapanda miti katika Shule mpya ya Queen Sendiga kwa lengo la kuimarisha mazingira na kufanya muonekano mzuri wa shule hiyo ya awali na Msingi.Pamoja na kukagua majengo ya ofisi,madarasa na vyoo vya shule hiyo. Amewapongeza wataalam na viongozi wote waliosimamia mradi huo.
Aidha Mhe. Sendiga amesema kuwa Mkoa wa Manyara umepokea fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya uboreshaji wa huduma za maji,umeme,barabara pamoja na vituo vya afya katika halmashauri zote zilizopo Mkoa wa Manyara.
Vilevile Mhe. Queen Sendiga amewataarifu wananchi kuwa Mkoa wa Manyara ni miongoni mwa Mikoa ya kimkakati katika uwekezaji katika sekta ya madini,kilimo na utalii ambapo amewaelezea kuwa Mkoa wa Manyara utafanya uzinduzi wa jarida maalum la uwekezaji terehe 10/10/2023.
Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amefanya ukaguzi wa ujenzi wa shule maalum ya Sekondari michepuo ya Sayansi kwa wasichana ya Mkoa wa Manyara.Katika ukaguzi wake ameonyeshwa michoro ya majengo katika ujenzi wa shule hiyo. Amefanya ukaguzi wa miundo mbinu ya maji ambayo itasaidia kutatua kero ya maji kwa wanakijiji wa kiongozi.
Pia ujenzi wa shule hiyo ni fursa kwa wakazi wa Kijiji cha Kiongozi katika ajira ambapo amesisitiza vijana katika kijiji hicho wapewe kipaumbele, wanawake wajasiriamali watumie vizuri fursa hiyo.Na ameomba eneo kwa Mwenyekiti wa kijiji kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.