Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga leo Septemba 19, 2023 amefanya kikao na wazee wa kimila na viongozi wa dini Mkoa wa Manyara. Kikao hicho kimeongozwa na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mhe. Dominic Mbwete katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa ambapo lengo la kikao hicho nikutambua umuhimu wa wazee na viongozi wa dini.
Mhe. Queen Sendiga ameomba ushirikiano wakutosha kutoka kwa wazee hao wa kimila na viongozi wa dini, ameongeza kuwa ili kutimiza majukumu ni lazima kuwe na mahusiano mazuri na wazee wa kimila na viongozi wa dini aidha amewahakikishia usalama wakutosha.
Pia ameeleza kuwa pamoja na mambo mazuri yanayo enedelea kufanyika katika Mkoa lakini kuna changamoto ambazo ni kukithiri kwa vifo vya boda boda katika Mkoa wa Manyara amewataka wazee hao wa kimila na viongozi wa dini kukemea maovu na mienendo mibaya kwa vijana.
Vilevile ameeleza juu ya suala la ukatili wa kijinsia amewataka viongozi wa dini na wa kimila kuisadia Serikali kuweza kuondoa tatizo hilo au kulipunguza. Akizungumzia suala hilo pia ametoa twakwimu fupi ya kuanzia Januari hadi Septemba 2023 ambapo Mkoa umeripoti kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia takribani 1628.
Amefurahishwa na uzalishaji wa zao la ngano kwa wingi Wilaya ya Hanang, ameeleza kuwa pamoja na kuzalisha chakula kingi lakini bado Mkoa unakabiliwa na tatizo na lishe. Aidha amesisitiza juu ya kuweka akiba ya chakula kwa wakulima ili kuepuka tatizo la kutokuwa na chakula cha kutosha.
Ametoa msisitizo katika suala la maadili kwa vijana huku akiwataka wazee hao wa kimila kuweka misingi ya malezi bora kwa watoto sambamba na hilo amewata wazee wakimila kutobebwa na utandawazi bali waendelee kuziendeleza mila na desturi.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.