Leo Novemba 10, 2023 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amefunga mafunzo maalumu na kukabidhi vyeti kwa waheshimiwa Madiwani na Wataalamu (Wakuu wa Idara) wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ yaliyofanyika tarehe 09 na tarehe 10 Novemba, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Mjini Katesh.
Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na kuendeshwa na wataalamu kutoka Chuo cha Uongozi Hombolo kilichopo Jijini Dodoma, yalikuwa na lengo la kuwajengea uwezo Waheshimiwa Madiwani na Wataalumu wa Halmashauri hiyo kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwemo Uongozi na Utawala bora, Sheria za uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Matumizi ya Vishikwambi kuendeshea vikao n.k.
Aidha Mhe. Mkuu wa Mkoa amesisitiza kudumisha Utawala bora kwa kutumia mafunzo hayo na ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa waheshimiwa Madiwani na ametaka mafunzo hayo yakatumike vizuri katika kusimamia miradi ya Maendeleo na kuongeza chachu ya maendeleo katika uongozi sambamba na usimamiaji mzuri wa fedha za miradi.
Mwenyekiti wa Halamashauri ya Hanang amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwakuweza kushiriki katika kufunga mafunzo hayo aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ameeleza kuwa mafunzo hayo yatakuwa yakiendelea kufanyika mala kwa mara.
Vilevile Mhe. Mkuu wa Mkoa amewashukuru Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ kwa ushirikiano waliouonyesha wakati wa Kilele Cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 na ameomba ushirikiano huo uendelee kwenye shughuli zingine ya Mkoa.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.