Ujumbe kutoka serikali ya Misri ukiongozwa na Waziri wa Kilimo na ardhi wa nchi hiyo Dkt Ezzidine Abu Stiet upo nchini kwa ziara ya siku mbili kwa ziara ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Ukiwa nchini ujumbe huo mbali na kuonana na viongozi wa Wizara ya kilimo, ulipata fursa ya kuonana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege ambapo ulimweleza Naibu Waziri juu ya azma yao ya kutaka kuwekeza katika sekta za kilimo, na ufugaji wa kuku.
Kwa mujibu wa Waziri huyo wa kilimo na ardhi, Serikali ya Misri ingependa kuwekeza mojawapo kati ya mazao makuu matatu ambayo ni ngano, mpunga au miwa.
Kwa upande wake Naibu Waziri Mhe.Kandege aliupongeza ujumbe huo kwa nia yao ya kuwekeza katika kilimo nchini.
Waziri huyo wa kilimo wa Misri alifuatana na Mkuu wa kituo cha utafiti wa kilimo cha Misri Dkt Mohamed Soliman Mohamed, Meneja Mtendaji wa mashamba ya ushirikiano katika nchi za kiafrika Dkt Maher El Maghraby na Mkuu wa sehemu ya utafiti wa ngano kutoka taasisi ya utafiti wa mazao Dkt Salah Abd El-Megied Makady.
Ujumbe huo pia uliambatana na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe.Abdulwafa, Afisa Ubalozi wa Misri Bwana Ahmed, Meneja wa shamba la ushirikiano Zanzibar Dkt Reda Abdallah Abdelaziz, na Afisa wa shamba la ushirikiano la zanzibar anayehusika na uhandisi wa kilimo Dkt Yoursry Abdelkawy Sahan.
Wengine ni bwana Abbas Ngwale kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Misri na Bi Elizabeth Rwitunga afisa dawati wa Misri, Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Na Mathew Kwembe, Majid Abdukarim,
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.