Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Charles Makongoro Nyerere amezindua kampeni ya upandaji miti Kijiji Cha Nakwa, Kitongoji cha Sumbi kata ya Bagara Wilaya ya Babati mkoani Manyara
Rc Makongoro amesema lengo ni kuhamasisha Umma wa wanamanyara umuhimu wa upandaji miti na kuitunza kwa ajili ya kuongeza huduma na bidhaa zitokanazo na miti, utunzaji wa mazingira, utunzaji wa vyanzo vya maji na kukabikiana na mabadiliko ha Tabia ya Nchi.
Aidha Mkoa umepanga Ili kuweza kukabiliana na uhalifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji holela wa miti Kila halmashauri ya wilaya/Mji inatakiwa kupanda miti Milioni 1.5 Kila mwaka ambapo Katika Katika Mkoa wetu tunapaswa kupanda miti Milioni 10.5 Kila Mwaka.
Pia Rc Makongoro amezindua Kampeni ya upandaji Miche 5,000 ya miti kuzunguka ziwa Babati na Katika Mashule inayowezeshwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Miss Jungle International , MVIWAMA kupanda Miti 500,000 Halmashauri ya wilaya Babati na Mbulu na (TANROADS) wakala wa Barabara kupanda miti 17,200 Katika Barabara zote wanazosimamia Mkoa wa Manyara
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.