Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mheshimiwa Makongoro Nyerere leo amekabidhiwa rasmi ofisi na analiyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mheshimiwa Joseph Mkirikiti katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara.
Akitoa hotuba kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mheshimiwa Mkirikiti ambaye amehamishiwa mkoani Rukwa amewashukuru wananchi wa Manyara kwa ushirikiano wao kwa kipindi kifupi alichokuwa kama Mkuu wa Mkoa huo.
“Napenda kuwashukuru wananchi wote wa Manyara kwa kushirikikiana na mimi katika kipindi change chote cha Ukuu wa Mkoa wa Manyara Pamoja na kuwa mimi ndiye nilikuwa Mkuu wa Mkoa niliyekaa kwa muda mfupi kuliko Wakuu wa Mikoa sita waliowahi kukaa Manyara” Alisema Mhe. Mirikiti.
Akionekana mwenye furaha san Mheshimiwa Mkirikiti alimpongeza Mhe.Makongoro Nyerere kwa kuteuliwa kwake kuwa miongoni wa Wakuu wa mikoa wa yenye eneo kubwa la kiutawala na kumtaka kushirikiana na makundi yote kuanzia ofisini hadi ngazi ya chini ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Manyara.
Pia alimueleza Mhe.Makongoro kuwa Mkoa wa Manyara kiasili ni mkoa wa wakulima na wafugaji kwani asilimia themanini na tatu ya uchumi wa Manyara unategemea kilimo na ufugaji na asilimia saba tu ndio shughuli zingine.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makongoro Nyerere Mkuu wa Mkoa wa Manyara alimshukuru Mheshimiwa Mkirikiti kwa kuja kumkabidhi kijiti cha uongozi na kumuahidi kuchapa kazi kwa ushirikiano mkubwa pamoja na kuwa hajawahi kuwa Mkuu wa Mkoa.
“Mhe. Mkirikiti mimi sijawahi kuwa Mkuu wa Mkoa ila nakuahidi kundeleza yote mema uliyoyaacha kwa kushirikiana na wasaidizi wangu kuanzia hapa ofisini hadi ngazi za chini na katika kipindi change cha uongozi sitegemei ubaguzi wa aina yoyote” Alisema Mhe. Makongoro Nyerere.
Mara baada ya makabidhiano hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bwana Musa Missaile pamoja na kumtakia kazi njema Mheshimiwa Mkirikiti huko aendako na kumuahidi ushirikiano Mheshimiwa Makongoro Nyerere aliwakabidhi viongozi hao zawadi mbalimbali ili kuweka historia ya ushirikiano na Viongozi hao.
Mheshimiwa Makongoro Nyerere amekabidhiwa ofisi leo baada kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara kuchukua nafasi ya Mheshimiwa Joseph Mkirikiti aliyehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Picha za matukio angalia kwenye maktaba ya picha.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.