Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Mkirikiti ameupongeza uongozi wa Kijiji cha Ngage kata ya Naberera wilayani Simanjiro kwa ujenzi wa vyoo bora ambavyo vitasaidia kuzuia magonjwa ya mlipuko
Mkuu wa Mkoa ametoa pongezzi hizo leo alipokuwa anatembelea na kukagua miradi ya Elimu ya EP4R na ujenzi wa vyoo bora Shule ya Msingi Ngage na kuzitaka kamati zote za ujenzi Mkoani Manyara kuiga uj
"Tangu nimeanza kutembelea kukagua miradi kwa kweli huu ni mradi bora sana, naziagiza Halmashauri zote zilizopo katika Mkoa wangu kuiga na kujenga vyoo bora kama hivi"Alisema Mhe.Mkuu wa Mkoa.
Pamoja na kuziagiza kamati zote za ujenzi kujenga vyoo bora ili wanafunzi kujiepusha na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu lakini pia Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa alimpongeza Mwalimu wa usafi shuleni hapo Bi. Plaxidia Stanslaus kwa usimamizi mzuri wa kuhakikisha vyoo vinakuwa safi muda wote.
Choo bora kilichojengwa katika shule ya Msingi Ngage.
Mkuu wa Mkoa kabla ya kutembelea shuke ya Ngage katika Wilaya ya Simanjiro alitembelea pia Shule ya Msingi Tanzanite,Songambele na Jitegemee kwa kukagua ujenzi wa madarasa na vyoo,katika Shule ya Jitegemee alifurahishwa na ujenzi wa madarasa katika shule hiyo na kuwataka wanafunzi katika shule hiyo kuhakikisha wanatunza miundombinu iliyopo ili iweze kuwasaidia Wanafunzi wengine kwa miaka mingi ijayo.
Hili ni miongoni mwa Darasa linalojengwa shule ya Msingi Jitegemee iliyopo Mirerani wilayani Simanjiro.
Pia Mheshimiwa Mkirikiti alipata nafasi ya kutembelea shule ya Msingi Losonokoi na kukagua ujenzi wa madarasa manne unaoendelea katika shule hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Mkirikiti akikagua daftari la Mwanafunzi shule ya Msingi Losonokoi wilayani Simanjiro.
Pamoja na kutembelea miradi ya ujenzi wa vyoo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa pia aligawa mpira wa miguu mmoja kwa kila shule aliyopita ili kukuza vipaji vya watoto katika Wilaya hiyo na kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Bwana Yefred Myenzi kupeleka Mpira ya pete katika shule hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Mkirikiti akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Songambele iliyopo Mirerani wilayani Simanjiro.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa yupo kwenye ziara ya kukagua miradi ya Elimu Mkoani humo na kesho atatembelea Wilaya ya Kiteto.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Songambele wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Mkirikiti (Hayupo pichani)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.