Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti (mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti amewataka Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Manyara kuhakikisha fedha zilitengwa kwa ajili lishe zinawafikia walengwa na kutumika ipasavyo kama miongozo inavyoelekeza. Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo Ijumaa 23 Julai alipokuwa akifungua na kuendesha kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kilichozungumzia juu ya tathimini ya nusu mwaka ya mkataba wa lishe kwa ngazi ya Mkoa na Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara.
Wakitoa malalamiko yao Maafisa lishe waliohudhuria katika kikao hicho walisema wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa sababu ya changamoto ya kutokupewa fedha za kuwahakikisha wanaondoa hali ya udumavu.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti akifungua kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao cha tathimini ya lishe Mkoa kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara 24 Julai,2020.
Akijibu hoja hiyo Mkuu wa Mkoa aliwaagiza maafisa wanaoshughulikia mipango na bajeti ngazi ya Halmashauri hasa Maafisa mipango na makatibu wa afya wa Halmashauri waache maafisa lishe wahusike moja kwa moja katika kupanga afua za lishe ndani ya mfumo ulioboreshwa wa PlanRep maana kumekuwepo na tabia ya kupunguza afua bila kuzingatia weledi na ndo maana afua hizo hazileti tija.
Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa aliwataka wajumbe waliohudhuria kuhakikisha wanawakumbusha wajumbe wa kamati zote kuanzia ngazi ya Mkoa,Halmashauri,Kata na Vijiji pamoja na viongozi wote kutoa kipaumbele kwa masuala ya lishe ili kuweza kupunguza kiwango cha udumavu katika Mkoa wa Manyara.
“Watoto 36 kati ya 100 wamedumaa Mkoani kwetu na hivyo hawana uwezo wa kufundishika na hata kuleta tija katika kuinua uchumi wa Taifa na badala yake gharama kubwa hutumika kuwatunza, kwa hiyo nawataka wahusika wote kuhakikisha tunapunguza kiwango cha udumavu katika Mkoa wa Manyara” Alisema Mhe.Mkirikiti.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti akiendesha kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao cha tathimini ya lishe Mkoa kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara 24 Julai,2020.
Vilevile alizitaka Halmashauri kuhakikisha masuala ya lishe yafanywe kama agenda ya kudumu kuanzia ngazi ya mkoa hadi kijiji na mtaa na ikiwezekana lipelekwe hadi Makanisani na Misikitini kwa waumini wasiokuwa na lishe nzuri hata kusikiliza mahubiri na kuelewa na vigumu.
Afisa Lishe Mkoa wa Manyara Bwana Mabula Masunga akitoa mada wa wajumbe wa kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao cha tathimini ya lishe Mkoa kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara 24 Julai,2020.
Katika Kikao hicho Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliwashukuru wadau mbalimbali wakiwemo GAIN ambao wamekuwa nguzo kubwa katika kuimarisha elimu ya matumizi ya chumvi yenye madini joto na Shirika la lisshe la kimataifa la “Nutrition International” wanaofadhili Mkoa wa Manyara katika uchakataji madini joto kwenye chumvi.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti akiendesha kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.
Baadhi ya wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Manyara waliohudhuria kikao cha tathimini ya lishe Mkoa kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara 24 Julai,2020.
Katika Kikao hicho Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imepewa zawadi ya cheti kwa kuwa wa kwanza katika kutekeleza mpango wa lishe ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti (kulia) akimkabidhi cheti cha ushindi Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Kanali Patrick Norbert Songea katika kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Kanali Patrick Norbert Songea (kulia) akiwa na Maafisa Lishe wa Wilaya hiyo baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi katika kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti (kulia) akimkabidhi cheti cha ushindi Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu katika kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Bi. Sarah Sanga (kulia) akiwa na Maafisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi katika kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.
Hiki ni kikao cha nusu mwaka cha lishe na Mkoa wa Manyara umekuwa ukitekeleza Nkataba wa lishe kila mwaka kwa utaratibu ulijiwekea ukishirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kutathmini ulivyotekeleza afua mbalimbali kulingana na viashiria na vigezo vilivyowekwa wakati wa kutia saini mkataba wa lishe.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti akiendesha kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti (mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.
Imeandikwa Na:Haji A.Msovu (Afisa Habari Mkoa wa Manyara)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.