Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Mkirikiti amezitaka taasisi mbalimbali za kifedha zilizomo Mkoani humo kutoa mikopo kwa makundi mbalimbali ya wenye ulemavu ili makundi hayo yapate mikopo na kuweza kujikwamua kutokana umasikini.
Aliyasema hayo jana katika warsha ya wajasiriamali ambao ni walemavu wa kusikia (viziwi) iliyoandaliwa na tume ya ushindani (FCC) ambayo ililenga kuwapa elimu ya kutambua na kuepuka kununua bidhaa bandia zinazozalisha na watu mbalimbali ambao hawana nia njema na jamii.
"Niwaombe taasisi za kifedha ziwazeshe wajasiriamali walevu ili waweze kunufauke kupitia vikundi vyao" Alisema Mhe.Mkirikikiti.
Pamoja na kuzitaka taasisi hizo za kifedha Mkoani humo Mhe.Joseph Mkirikiti ameeleza kuwa mtu anayetengeneza bidhaa bandia anakusudia kupata faida kubwa na asiyostahili na ndio maana hazingatii vigezo na masharti katika utengenezaji wake na wamekosa uzalendo kwa nchi pamoja na watu wake hivyo serikali haikubaliani nao.
Alisema kuwa mtu ambaye anazalisha bidhaa bandia haishii tu kukosa uzalendo bali anadhamira ya kukwepa kodi hali inayopelekea kudhoofisha uwezo wa serikali katika kuwahudumua watu wake na jambo hilo maana yake siyo kuathiri tu watumiaji wa bidhaa hizo kwa sasa bali anaathiri na kizazi kijacho hivyo ni lazima kuunganisha nguvu zetu kukataa huduma za namna hiyo.
“Na nyie kwasababu ni wajasiriamali hamna budi kwa bidhaa zile ambazo mnashiriki kuzitengeneza najua mnaweza kutengeneza sabuni za maji na wengine mnatengeneza bidhaa za mapishi kama mafuta na viungo ni vizuri mkaepuka matumizi ya bidhaa ambazo hazina ubora na pia jengeni mazoea ya kutumia viungo vyetu vya ndani ambavyo ndio vinaubora zaidi,
“Zaidi sana niwaombe wazalishaji wa bidhaa zote bandia zinazotumika na wanadamu kuacha kuzitengeneza nchi yetu siyo eneo la kutupa takataka,watanzania siyo watu wa kutumia bidhaa za hovyohovyo”alisema Mkirikiti.”
Naye Mkurugenzi Mkuu wa tume ya ushindani na uthibiti wa bidhaa bandia Godfrey Mshana alieleza kuwa semina hiyo ni mhimu kwa Mkoa wa Manyara kwani ni miongoni mwa Mikoa ya pembezoni ambayo endapo itakabiliwa na changamoto za bidhaa bandia watu wengi wataathirika kabla ya changamoto hiyo haijapatiwa uvumbuzi .
Elimu ni silaha bora zaidi ya kuweza kupambana na bidhaa bandia kuliko hatua za utekelezaji wa sheria ambayo huchukua muda wa matunda yake kuonekana.
Alisema kundi la walemavu ni kundi muhimu kupewa ulinzi wa kipekee dhidi ya athari za bidhaa bandia kwa ni lina mahitaji maalumu hivyo unapolifikia kundi hilo kwenye masuala ya elimu unakuwa umewafikia wananchi wote.
“Katika siku zijazo tume ya kuthibiti bidhaa bandia inafikiria namna bora na yenye ufanisi zaidi ya kupeleka elimu kwa makundi maalum ya walemavu hususani wenye ulemavu wa kusikia na kuona kwa kuwa ndi mafunzo yenye changamoto na uhitaji mkubwa wa elimu ya jinsi ya kuthibiti na kuepuka bidhaa bandia”alisema Mshana.
Neto Mhadisa ambaye ni mshiriki wa mafunzo hayo ambaye pia ni katibu wa chama cha visiwi Mkoa wa Arusha visiwi wengi wamekuwa wakishindwa kutambua bidhaa feki kutokana na kutokuwa na elimu huku akisisitiza kuwa viziwi wengi hwajui kusoma hivyo inawawia vigumu kutambua kama ni bidhaa feki.
Aliomba pia Mkuu wa Mkoa kuweka mkalimani katika ofisi yake ili watu wenye ulemavu wa kusikia waweze kupata huduma katika ofisi yake kwani tatizo kubwa lipo kwenye mawasilano na wao kama viziwi wanatumia lugha ya alama ambayo watu wengi hawajui kuitumia.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.