Maadhimisho ya wiki ya elimu mkoa wa Manyara ya lifikia kilele siku ya jumatano tarehe 15/8/2018 katika wilaya ya Babati viwanja vya kwaraa.
Akitoa salamu za utambulisho Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati Bw. Salum Issa alisema kuwa maadhimisho hayo yamelenga kuhamasishana, kuelimishana na kutoa elimu juu ya uwajibikaji kwa pamoja kati ya walimu ,wazazi na wanafunzi katika kufanikisha mpango wa elimu bora.
Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi Kaimu Afisa elimu mkoa wa Manyara Bw.Lago Silo alisema kuwa mkoa wa Manyara una shule za msingi 640,shule za serikali 601na shule binafsi zipo 39 halikadhalika shule za sekondari zipo 156,shule za serikali139 na shule za binafsi zipo18 ambazo zina jumla ya wanafunzi 304,677 kwa shule za msingi na 52008 wa shule za sekondari. Kutokana na mtawanyiko wa kijographia ambao unaamuliwa na shughuli za kijamii ambapo mkoa una shule za msingi za bweni hii ni kwa sababu kuna jamii za kifugaji zinazohitaji huduma za shule za bweni ambapo alisema wilaya ya hanang ina shule 4, kiteto7,simanjiro3 ,mbulu2 na babati shule 3.
Pia alisema maendeleo ya kitaaluma katika mkoa huo yanaboreka kila mwaka hasa ukizingatia matokeo ya darasa la saba kwa miaka mine mfululizo 2013 yalikuwa ni asilimia ( 42.4), 2014 (48),2015 (59.18) na pia katika mtihani wa kumaliza kidato cha nne ufaulu umeongozeka kutoka asilimia 62 ya mwaka 2016 na hadi asilimia 82 ya mwaka 2017 na mtihani wa kidato cha sita kutoka asilimia 92 hadi asilimia 99 kwa mwaka huu wa2018 ambapo alisema kiwango hiki hakiridhishi hivyo jitihada zinaendelea ili kufaulisha kwa asilimia 100 kwa kila mitihani.
Katika uboreshaji wa elimu serikali iliamua kubuni program ya lensi ili kuboresha elimu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi ambapo katika elimu ya msingi imejikita katika kukuz a stadi za kusoma ,kuandika na kuhesabu ili kuwajengea walimu umahiri na ujuzi wa kufundisha stadi hizo na kuboresha mtaala na miongozo katika kufundisha na kuzungumza stadi hizo.
Kwa kupitia program ya lensi mkoa wa Manyara umefanikiwa kuwapatia mafunzo kamati maadili za shule, mafunzo kwa ajili ya walimu wapatao 2919 wa darasa la awali ,la kwanza,pili,la tatu na la nne,pia usambazaji wa machapisho ya vitabu vya kiada na ziada, mihtasari na miongozo katika kufundishia na fedha kwa ajili ya ufatiliaji wa takwimu kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa pia wanafunzi wenye mahitaji maalum ambapo jumla ya sh. Million 32,800,090 zilitumika.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw. Kennedy Kaganda katika hotuba yake alisema kuwa ”nimefurahishwa na maonyesho ya kwenye mabanda, nyimbo na ngoma ambazo zimebeba ujumbe muhimu wa siku ya leo kwani inaonyesha jinsi gani walimu wamejikita kuhakikisha elimu bora kwa wanafunzi inapatikana na pia wanafunzi walio shinda katika mashindano ya usomaji wa darasa la pili na la tatu ni dhahiri kwamba ni wajibu wetu sote wazazi, walimu na wanafunzi kushirikiana katika kuboresha maendeleo ya kielimu katika mkoa wetu ,Wazazi washirikiane na walimu katika kufatilia maendeleo ya kielimu ya motto hasa wahakikikishe wanakwenda shule, pia wanafunzi wajitambue kwani elimu ndio msingi wa maisha alisisitiza.
Akijibu changamoto mbalimbalizi lizojitokeza katika taarifa ya lensi alisema mkakati wa kuongeza shule na madarasa ni jukumu la serikali lakini pia mchango wa wananchi una nafasi kubwa katika maendeleo ya kijamii na katika swala la upugufu wa vitabu, ukosefu wa mafunzo kwa walimu na upungufu wa walimu alisema kuwa wawe na subira kwani serikali inatoa fedha na ajira kwa awamu .
Maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa yalijumuisha Halmashauri saba za mkoa huo ambazo ni Halmashauri ya wilaya ya Babati, Babati mji, Simanjiro, Kiteto, Mbulu wilaya, Mbulu mji na wilaya ya Hanang,
KAULI MBIU YA MWAKA HUU ni “Uwajibikaji wa pamoja katika kutoa elimu bora”
Imeandikwa na: Isabela Joseph (Mwanafunzi wa UDSM(SJMC)- Mafunzo kwa vitendo)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.