Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akizungumza na Wenyeviti na watendaji wa Mitaa na vijiji, amewataka kuacha tabia ya kulalamika kwa viongozi pindi wanapofika kwenye maeneo yao, na badala yake wawe wa kwanza kuzitatua changamoto hizo kwa kuwa wao na yeye wanafanya kazi .
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Viongozi hao kutoka wilaya na Halmashauri zote za mkoa wa Manyara,kikao kilichofanyika katika uwanja wa ofisi ya mkuu wa mkoa mtaa wa Komoto Babati mjini.
Baadhi ya Maafisa Tarafa, watendaji wa kata, Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji, Watendaji wa Mitaa na Vijiji kutoka Mkoa wa Manyara wakiwa katika Mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Manyara uliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Januari 14, 2020.
Aidha, Mnyeti amesema hafurahishwi kusikia malalamiko ya mara kwa mara anayokutana nayo kutoka kwa wananchi wakati anapokuwa kwenye ziara mbalimbali za kikazi mkoani mwake, huku matatizo mengi yakiwezekana kutatulika katika ngazi za Kijiji au Mtaa.
Akiwashauri Wenyeviti hao njia bora ya kuwahudumia wananchi na kuondoa migogoro ya ardhi, Mnyeti aliwataka waache tabia ya kuuziana maeneo bila kufuata taratibu na ushauri wa mtendaji pamoja na kuepuka kuuza maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya shuguli mbalimbali za kijamii.
Amesema kila kiongozi akitimiza wajibu wake kama inavyopaswa mkoa wa Manyara hautakuwa na migogoro isiyo na maana.
Baadhi ya Maafisa Tarafa, watendaji wa kata, Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji, Watendaji wa Mitaa na Vijiji kutoka Mkoa wa Manyara wakiwa katika Mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Manyara uliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Januari 14, 2020.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.