Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Mh Karolina Mthapula 9/8/ 2023 ameendesha kikao cha mradi wa utafiti wa soko la sodo.
kikao lichoandaliwa na mashirika mawili yasiyo ya kiserikali OIKOS na Shirika la E-MAC mashirika yanayo jihusisha na mradi wa taulo za wanafunzi wa kike. Mradi ambao umefadhiriwa na Benki ya dunia (WORLD BANK), kikao hicho kimefanyika katika ukumbi namba 83 eneo la ofisi za Mkuu wa Mkoa.
Halmashauri mbili pekee ndizo zimehusishwa katika kikao hicho (Kiteto na Babati), Halmashauri hizo zikiwa ndio Halmashauri za mwanzo kuweza kupokea mradi huo wa utafiti.
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho Katibu Tawala Mkoa wa Manyara ameshukuru mashirika hayo OIKOS na E-MAC pamoja na wizara ya Afya kwakuleta mradi huwo wa utafiti kwakusaidia suala la sodo kwa mabinti wakike mashuleni.
Amewataka watu kuwapa ushirikiano wakutosha kwa mashirika hayo OIKOS na E-MAC ushirikiano ambao utaweza kurahisisha ufanikishaji wa mradi huo.
Pia amesisitiza suala la hedhi salama ni suala la kitaifa ambalo kila mtu kwenye jamii kulichukulia katika uzito, ameeleza kuwa ufanikishaji wa mradi huwo utakuwa umesaidi Taifa, ‘’hivyo kuna kila sababu ya kushukuru mashirika ya OIKOS na E-MAC’’ nukuu ya maneno ya Mh Karolina Mthapula (katibu Tawala Mkoa wa Manyara).
Aidha ameeleza ukosekanaji wa sodo unaweza kukatisha ndoto za mambinti wengi, Pia ameeleza kuwa kufanikiwa kwa mradi huo kutasaidia kuongeza mahudhurio shuleni kwa mabinti wengi.
‘’kuwa na sodo mashuleni kutasaidia kupunguza magonjwa na athari za kiafya’’ Ameweka wazi kuwa ofisi ya Mkoa ikotayari kutoa ushirikiano wakutosha kwa mashirika hayo OIKOS na E-MAC.
Asisitiza juu ya utolewaji wa elimu kwa watumiaji wa sodo yaani mabinti kwakuwa mabinti wanatoka katika mazingira tofauti, kuna watumiaji ambao kimsingi wanatoka mazingia ambayo bado uwelewa uko chini na wengine uwelewa wao ni mpana kuhusu utumiaji wa sodo.
kwakuzingatia hilo Katibu Tawala Mkoa wa Manyara ambae ndiye alikuwa mgeni rasimi katika kikao hicho ameweka msisitizo kwenye hilo.
Katika kikao hicho Afisa Elimu Mkoa ameeleza juu ya ukosefu wa sodo na jinsi unavyoweza kuchangia mahudhurio mambaya mashuleni, Nakupelekea baadhi ya mambinti kutofauru vizuri masomo na malanyingine wengine wanafanikiwa kwenda mbele lakini kutokana na tatizo la ukosefu wa sodo bado wanakuwa sio wataalamu wazuri.
Afisa Afya Mkuu wizara ya Afya ameeleza umuhimu wa Afya kwa akina mama wa badae ikiwa ni kuongeza uwelewa kwa jamii, ambapo ameeleza juu ya kaulimbiu ya wizara ikiwa ni uchochezi mkubwa wa kila mtu kwenye jamii.
‘’TUVUNJE UKIMYA’’
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.