Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu amewaomba wananchi wajitokeze kwa katika kuupokea Mwenge wa Uhuru unaoatajiwa kufika katika wilaya hii septemba 19 na kupokelewa katika kijiji cha Olasiti mpakani mwa Arusha na Manyara.
Aidha amewataka wananchi kuutunza Mwenge huo ambao utazunguka katika wilaya ya Babati kwa siku tano.
Akizungumza na Muungwana Blog ofisini kwake Dc Kitundu amesema katika Halmashauri ya wilaya ya Babati Mwenge utapokelewa kesho jumatano tarehe 19 na utazunguka hadi tarehe 23 utakapokesha katika kijiji cha Galapo kisha utapokelewa katika kijiji cha Sigino Halmashauri ya mji wa Babati na utakesha katika uwanja wa Kwaraa.
“Tumejipanga vizuri kuupokea mwenge wa uhuru mwaka 2018,maandalizi yote yapo tayari kwa Halmashauri zote mbili,kwa hiyo tupo vizuri na wananchi wote tunawakaribisha kuupokea mwenge kwa furaha”alisema mkuu wa wilaya.
Mwenge wa uhuru mwaka huu katika wilaya ya Babati utazindua na kukagua miradi kumi ambayo mitano ipo katika halmashauri ya Mji na mitano Halmashauri ya wilaya Kisha kukabidhiwa katika wilaya ya Kiteto tarehe 24.9.2018.
Ujumbe wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu ni Elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya taifa letu.
Imeandikwa Na: John Walter
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.