Mwenge wa uhuru umeingia katika mkoa wa MANYARA ukitokea SINGIDA ambapo utakimbizwa Katika Halmashauri zote SABA za wilaya TANO za mkoa huo ambapo utakimbia kilomita 980.5 kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 57 ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 149.5.
Akipokea Mwenge wa uhuru katika kijiji cha GEHANDU kwenye viwanja vya shule ya sekondari MWAHU Wilayani HANANG kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa SINGIDA HALIMA NDENDEGO, Mkuu wa mkoa wa MANYARA QUEEN CUTHBERT SENDIGA amesema kati ya miradi hiyo, shilingi milioni 837 ni michango ya Wananchi na milioni 500 ni michango kutoka wadau wa Maendeleo.
Amesema miradi 17 yenye thamani ya shilingi Bilioni 134.1 itawekewa mawe ya msingi, miradi 8 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.4 itazinduliwa, miradi minne yenye thamani ya shilingi 1.3 itakaguliwa na kuonwa na kutembelea miradi 28 ya yenye tamani ya shilingi milioni 10.7
Sendiga amesema kati ya fedha hizo nguvu za wananchi ni shilingi bili 102. 5 serikali bilioni 72.8 Halmashauri shilingi 169.7 wadau wa Maendeleo shilingi 76.5.0
Baada ya kuupokea SENDIGA amekabidhi Mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa wilaya ya HANANG ALMISHI HAZALI ambapo umekimbizwa kilimita 130 itatembelea miradi 9 yenye thamani ya shilingi bilioni 12.522.
Kwa mujibu wa Almishi Hazali miradi iliyokaguliwa na kuwekewa mawe ya msingi na mwenge wa uhuru Wilayani HANANG ni pamoja mradi mkubwa wa maji wa Mogitu GEHANDU utakaonufaisha watu 25 uliotekelezwa na serikali kupitia wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini RUWASA wilaya ya HANAN.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Hanqng mhandisi Hubert Kijazi mradi huo wa Mogitu-Gehandu unatekelezwa kwa awamu tatu kwa jumla ya shilingi Bilioni nane.
Akizungumza baada ya kuzindua miradi hiyo, kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2024 GODFREY MZAVA amepongeza RUWASA kwa kusimamia mradi huo na kufuata maelekezo ya serikali ya kutangaza zabuni kwa njia ya kidigitali na pia kuangalia uwezekano wa kupunguza bei ya maji kwa wananchi wa HANANG.
Miradi mingine iliyokaguliwa na kuwekewa mawe na msingi na mwenge wa uhuru ni pamoja jengo la mama na Mtoto katika hospitali ya wilaya ya HANANG ya Tumaini pamoja na ujenzi wa madarasa mapya matatu katika shule ya sekondari KATESH.
Mwenge wa uhuru hapo kesho utaendelea na mbio zake katika Halmashauri ya wilaya ya MBULU kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.