Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi ,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mh. William Ole-Nasha(MB) amefanya ziara ya kikazi leo tarehe 8,Oktoba Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara na kutembelea chuo cha ufundi stadi(VETA) na kituo cha elimu ya watu watu wazima(BTS) na dhumuni kubwa ya ziara yake ni kutembelea miradi ya wizara na pia kufatilia utendaji kazi wa watendaji wa serikali katika kitengo cha elimu .
Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi Afisa elimu Mkoa wa Manyara Bw. Anorld Msuya alisema zipo changamoto mbali mbali zinazoukabili Mkoa ikiwemo uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza ,hii ni kutokana na hamahama ya wanajamii hasa wafugaji, umbali wa maeneo ya shule kutoka kwenye makazi,uchakavu wa miundo mbinu ,uhaba wa walimu na upungufu wa madarasa mbali na changamoto hizo Mkoa unajitahidi kuhakikisha kila Halmashauri inakuwa na miundo mbinu bora ya kielimu ikishirikiana na wananchi na kuhakikisha kila tarafa iwe na shule ili kuhakikisha wanafunzi wanaopata elimu bora.
Akijibu taarifa ya Afisa elimu Mh. Naibu waziri alisema miundo mbinu ya kielimu bado inasikitisha na jukumu la serikali za mitaa kushirikiana na wananchi kuboresha miundo mbinu na pia maafisa elimu mnapaswa kutumia sheria ya serikali kuzidi kuwahamasisha wananchi kuwapeleka watoto shule aidha katika maeneo ambayo kuna mtawanyiko wa wananchi ni lazima muwe wabunifu kwa kujenga shule za bweni ,pia alisema “niwaombe watendaji wa serikali kutojijengea dhana ya kuunda magenge ya wizi wa mitihani suala ambalo sisi kama serikali hatutaliunga mkono”.
Vilevile katika ziara yake Mh.Ole- Nasha alipotelembelea chuo cha ufundi stadi ( VETA -MANYARA) alitoa fursa kwa wanafunzi kuelezea changamoto na matarijo yao katika kozi wanazozisomea wanafunzi hao walisema mafunzo wanayopatiwa ni mazuri lakini bado wanakumbana na changamoto ya uhaba wa walimu na ajira mitihani hivyo wanaiombana serikali iwasaidie.
Akitoa hotuba katika ziara yake alijibu hoja za wanafunzi hao Mh. Naibu Waziri alisema “ serikali imejipanga kuboresha ngazi mbali mbali za elimu kuendana na teknolojia ya kisasa,ili kuendesha uchumi wa viwanda nilazima uwe na nguvu kazi ya ufundi hata hivyo bado tunaendelea kupanua wigo w afursa kwa wananchi wengi kwenda shule na ni jukumu lenu kwenu wanafunzi kujijengea dhana ya kujiajiri kama sera na mtazamo wa serikali unavyosema “ alisistiza aidha serikali bado inavitambua na kuvithamini vituo vya elimu ya watu wazima kwani ni jukumu la kila mwanachi kupata elimu bora.
(Kwa Picha mbalimbali angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Imeandikwa na Isabela Joseph (UDSM-Mafunzo kwa Vitendo)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.