Naibu waziri wa elimu Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya ufundi Mh. William Ole-Nasha amaeitaka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kutumia fedha za serikali vizuri ili kuhakikisha miradi ya kimaendeleo ya kielimu inakamilika kwa wakati bila kuwepo changamoto yoyote.
Aidha akikagua majengo ya shule zilizopo Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara ambazo ni Nangwa na Endasak Mh. Waziri aliitaka Mamlaka ya Elimu Tanzania kutumia utaratibu au mfumo wa FORCE- ACCOUNT ili kujenga majengo yenye ubora na kwa bei nafuu ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi. Mh Waziri aliisisitiza mamlaka hiyo kutumia mfumo huo katika uratibu ambapo alisema “ watumie (force account) kwa njia ya manunuzi ya kupunguza gharama za ujenzi kupitia usimazi wake na kamati za ujenzi , wataalam wa ngazi ya Wilaya kwa kupitia mafundi wa kawaida na siyo wakandarasi wakubwa”.
Vilevile alitoa magizo kwa wakandarasi wa ngazi zote anaopewa tenda za kujenga majengo hayo kufuata maelekezo ya Wizara ya elimu ikiwemo michoro ya ramani za majengo na fedha zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi ili fedha zitumike kwa ufasaha bila kupatikana changamoto yoyote au kutokukamilika kwa mradi kwani kutokufata maelekezo ni kukiuka maagizo ya serikali.
Awali mkuu wa Wilaya hiyo Mh.Joseph Mkirikiti aliitoa shukrani zake kwa serikali ya awamu ya tano pamoja na wizara ya elimu kwan wao kama Wilaya ni wanufaika wa miradi hiyo na wamejipanga kuhakikisha inakamilika kwa wakati ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi na jamii inayowazunguka ambapo ni wakereketwa wa kielimu na pia aliahidi kuendelea kushirikiana na wakandarasi na kamati ya jenzi wa shule hizo ili kuhakikisha majengo hayo yanajengwa katika kiwango cha ubora kama wizara ilivyoelekeza.
Akihitimisha ziara yake katika shule hizo Mh Waziri alisema serikali ya awamu ya tano imejikita kuboresha miundo mbinu ya kielimu na kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki na bora ikiwemo kuta fedha za ujenzi vifaa na kuboresha miundo mbinu ili kuleta maendeleo nchini.
(Kwa Picha mbalimbali angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Imeandikwa na Isabela Joseph (UDSM-Mafunzo kwa Vitendo)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.