Naibu Waziri Mh.William Ole -Nasha ametoa agizo hilo kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakamilisha miradi ambayo fedha zake zilitolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya kielimu.
Mh.Ole-Nasha alitoa agizo hilo katika Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Mji wakati akikagua mradi wa ujenzi wa mabweni, madarasa na vyoo katika shule ya sekondari ya Chief Sarwatt iliyopo katika Kata ya Endagikot ambapo mradi huo wa ujenzi haujakamilika na fedha za serikali kuwa zimekishwa. Mh. Waziri alitoa rai viongozi wa serikali pamoja na kamati ya ujenzi wa shule hiyo kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya miezi mitatu tu.
“kwasababu wataalam wa Halmashauri ndio wametuchelewesha kukamilisha mradi ni lazima muhakikishe fedha inapatikana ili mradi ukamilike,ikiwemo kuwahamasisha wananchi kuwaunga mkono kwa kuchangia fedha za ujenzi ili majengo hayo yatumike kwa kwakati kama wizara ilivyoelekeza” alisisitiza Mh.Waziri
Aidha alisema kutokufuata maelekezo ya wizara kunachelewesha miradi mingi kutokamilika na fedha kutumika vibaya na hii husababisha kutikidhi mahitaji ya wanafunzi wengi kwawakati mmoja. Vile vile alipotembelea shule ya sekondari Gehandu ambayo ujenzi wake ulikuwa unaanza alitoa rai kwa viongozi pamoja na kamati ya ujenzi kuhaikisha makosa hayafanyiki tena kama ilivyotokea katika miradi mingine na pia aliwasifu wananchi wa eneo hilo kuwa na wapaenda maendeleo kwani sehemu kubwa ya ujenzi ni nguvu za wananchi.
Akiunga hoja ya Mh.Ole-Nasha Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mh. Chelestine Mofuga ameahidi kuwa sehemu ya kamati hiyo ya ujenzi na kuhaidi kutoa msaada wa kimawazo na ushauri ili makosa yasitokee na kuchelwesha mradi kukamilika na kuahidi kufanya vikao na wahandisi pamoja na wakandarasi ili kuhakikisha fedha zilizoletwa na serikali katika mradi huo zinatumika kama Wizara ilivyoelekeza kwa kufuata ramani na michoro ya majengo ambayo yatakidhi viwango vya ubora na mahitaji ya wanafuzi kutokana na idadi yao.
Naibu Waziri pia alitembelea chuo cha maendeleo ya wananchi (TANGO) ambacho kiko katika mpango wa serikali wa awamu ya tatu ya kukifanyia ukarabati wa majengo,miundombinu pamoja na vifaa vya kujifunzia aliwataka wanafunzi kuwa wavumilivu na serikali yao iko pamoja na wao ili kuhakikisha chuo hicho kinakidhi viwango kama vyuo vingine,na kuwasihi kuwa na bidii uwajibikaji uzalendo na kujijengea dhana ya kujiajiri ili kuendana na soko la ajira katika kipindi cha karne ya sayansi na teknolojia.
(Kwa Picha mbalimbali angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Imeandikwa na Isabela Joseph (UDSM-Mafunzo kwa Vitendo)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.