Naibu waziri wa Maji Jumaa Aweso amemuagiza Katibu Mkuu wawizara ya Maji kutoa kibali cha kufanya tathmini ya eneo la chanzo cha maji cha Bonga wilayani Babati mkoa wa Manyara ili mradi uweze kukamilika na wananchi walipwe fidia kupisha mradi huo.
Alitoa agizo hilo leo katika ziara yake mkoani Manyara iliyoanza leo yenye lengo la kukagua utekelezaj wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa sekta ya maji katika wilaya ya Babati.
Pamoja na utekelezaji wa miradi ya maji serikali inatambua kuwa inapowekeza katika miradi ya maji wakati mwingine utekelezaji wa miradi inapita katika makazi ya watu maana yake inaathiri makazi ya watu alisema wizara itahusika katka kulipa watu watakaostahili kulipwa.
“Wasiostahli hulipwa hawatalipwa tutafanya tathmini lakini kwa wale ambao wanashahili kulipwa tutawalipa na wawe ambao hawashahili kulipwa hatutowalipa, waheshimiwa madiwani na wabunge naomba msimamie hilo katika kuhakikisha mradi huu haukwami”
Alisema wananchi wa Babati na Manyara kwa ujumla wamelilia kilio cha maji kwa muda mrefu ambapo amejiridhisha kuwa tatizo la maji lipo na serikali inaleta fedha nyingi katika kuhakikisha inatatua tatizo la maji aliwataka kuitunza miradi ya Maji ili iweze kudumu.
Pamoja na utekelezaji wa miradi ya maji alielekeza ajira zitolewe bila upendeleo,ukabila na kujuana bali zitolewe kwa wananchi wenye sifa ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa mkandarasi mwenye uwezo wa kifedha wakuweza kutekeleza na ujuzi katika kuhakikisha miradi hiyo haikwami kwani wizaraya Maji haitakuwa kikwazo katika kuhakikisha wakandarasi wanalipwa fedha kwa wakati.
Naibu Waziri Awesu pia alikagua miradi ya maji ya kisima cha Haraa,Tsamas na Minjingu wilayani Babati katika Mradi wa maji wa Minjingu ulioshindwa kukamilika kwa wakati na kuitaka serikali kutenga tena fedha na alitoa agizo la kukutana na mhandisi na mkandarasi aliyehusika.
(Kwa picha mbalimbali angalia sehemu ya Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Imeandikwa na: Haji A.Msovu
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.