Maonesho ya kilimo na Wafugaji Kanda ya Kaskazini yanayofanyika Mkoani Arusha katika viwanja vya Themi yamevutia watu wengi sana wa mikoa ya Manyara ,Arusha na Kilimanjaro kutokana na wafugaji,wakulima na wafanyabiashara mbalimbali kujitokeza katika maonesho hayo na kuonesha bkidhaa zao kwa wananchi.
Akikagua mabanda ya Kilimo Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mh. Iddi Hassani Kimanta alifurahia maonesho hayo na kuzitaka Halmashauri zote katika Kanda ya Kaskazini kulete wakulima na wafugaji kwenye maonesho hayo ili kujifunza mambo mbalimbali na kupeleka ujuzi watakaoupata kwenye jamii wanazoishi ili kujikwamua na umaskini.
“Nimevutiwa sana na jinsi Halmashauri ya Wilaya ya Moshi walivyoanzisha Kilimo cha Vannila kwani kinaongeza kipato sana na pia unaweza kupanda mazao zaidi ya moja kwenye shamba moja kwa mfano Migomba au Kahawa na Vannila” Alisiistiza Mh.Kimanta
Pamoja na kuvutiwa na Ukulima wa wa Vannila pia aliona jinsi Halmshauri hiyo ilivyowafundisha wakulima wake kutumia eneo dogo kupanada mazao ya mbogamboga mengi na kuongeza kipato cha familia “Hii unaweza kupanda mboga katika sehemu ndogo ukapata mboga ya nyumbani, ukafanya biashara na pia ikawa ni sehemu ya Bustani kwa ajili ya kupamba Nyumba” Aliongeza Mkuu wa Wilaya ya Monduli.
Pamoja na kuonan shughuli hizo pia aliona jinsi ya uvunaji, usindikaji na upakiaji wa asali unavyofanyika katika njia bora na kuliongezea thamani zao la asali kwenye Banda la Waziri Mkuu Msaatafu Mh.Mizengo Pinda na kuwataka wafugaji na wasindikaji wengine wa asali waende wakijifunze kupitia banda hilo.
Vilevile Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli alijionea jinsi wajasiriamali Vijana kutoka Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro walivyoeweza kutumia mbinu rahisi ya ufinyangaji wa vyungu na Wasusi kutoka Halmashauri ya Mji Mbulu wanavyotumia malighafi zilizopo katika maeneo yao kutengeneza mikeka inayodumu kwa muda mrefu bila kuchafua mazingira.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Monduli alitembelea mabanda ya Kusindika Asali kutoka Katavi kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Pinda,Panda la World Vision, mabanda ya Kilimo kutoka Halmashauri za Moshi Wilaya,Mwanga,Same,Rombo,Longido,Mbulu Mji na Monduli.
Wakijumuisha maonesho kwa siku ya Jana Wakuu wa Wilaya ya Monduli,Same na Monduli waliishauri kamati ya Maandali kutenga siku maalumu kwa kila Mkoa iliyomo kanda ya Kaskazini kuja kuonesha mambo mbalimbali ya kiutamaduni yanayofanywa katika mikoa yao.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandali ya Nane Nane Kanda ya Kaskazini Anza-Amen Ndossa alisema kuwa watayafanyia kazi yale yote yaliyopendekezwa na kutolewa ushauri na wageni waliotembelea Manoneshoi hayo kwa siku ya jana na siku zote ili kuboresha zaidi msimu ujao.
(Kwa picha mbalimbali angalia sehemu ya Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.