Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara imekabidhiwa tuzo ya Afya ya usafi wa mazingira baada ya kushika nasafi ya kwanza katika mashindano ya Afya na usafi wa mazingira ambazo zilijumuisha ofisi zote za wakuu wa mikoa Tanzania bara.
Akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo hizo ambazo zinatolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Alexander Mnyeti Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bw. Missaile Musa amesema kuwa Ofisi ya Mkoa imezawadiwa cheti cha afya na usafi wa mazingira,Ngao na Fedha Taslimu kiasi cha shilingi Milioni tatu kutokana na kuyatunza mazingirz katika hali ya usafi na kuyaboresha zaidi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara amekabidhi cheti cha Afya na usafi wa mazingira, hundi ya shilingi milioni tatu, ngao na cheti cha ufanisi kupitia mazingira na kuwataka wafanyakazi waimarishe usafi zaidi.
Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Alexander Mnyeti amewapongeza wafanyakazi wote katika ofisi yake kwa kupata tuzo hiyo.
“Mkoa wa Manyara uko vizuri katika kila sekta sio tu kwa upande wa mazingira nataka kila mfanyakazi afanye kazi kwa bidii mkoa wetu tunafanya kazi hatupigi kelele nawatakia sikukuu njema ya kupokea mwaka mpya wa 2020”Amesisitiza Mh. Mnyeti.
Tuzo ya Afya na usafi wa mazingira zimekuwa zikitolewa kila mwaka kwa ofisi za wakuu wa mikoa wa Tanzania bara kwa lengo la kuomgeza ufanisi na kuimarisha usafi wa mazingira.
(Kwa picha mbalimbali angalia sehemu ya Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.