Kamati ya maafa Mkoa wa Manyara leo Jumatatu tarehe 24/02/2020 imepatiwa mafunzo na Waratibu wa maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ya jinsi ya kujikinga na kudhibiti maafa pindi yanapotokea.
Akifungua mafunzo hayo Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bwana Missaile Musa aliwataka washiriki wa mafunzo kufuatilia na kushika kila wanalofundishwa na wataalam hao ili kuweza kufikisha utaalam huo kwa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya kata hadi ya Halmashauri ili Jamii za Mkoa wa Manyara ziweze kupata elimu na kuweza kukabiliana na maafa pindi yatokeapo.
“Nawahusia washiriki wote wa mafunzo haya mfuatilie kwa makini ili myapeleke kwa jamii zetu ili jamii hizo ziweze kujifun za namna ya kukabiliana na maafa” Alisema Katibu Tawala.
Akiwasilisha mada Mratibu wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bwana Harrison Chinyuka amesisistiza kwa kamati kutoa mafunzo kwa kamati za Wilaya, Halmashauri, Kata hadi ngazi ya Jamii juu ya kujikinga kuliko kudhibiti katika maeneo yao kwani kujikinga kunapunguza gharama kuliuko kudhibiti.
“Kila Idara,na kila mwananchi ana jukumu la kushughulikia maafa na tukitoa elimu kwa kiwango cha hali ya juu maafa yatapungua kwakiasi kikubwa mno” Alisema Bwa Chinyuka.
Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Manyara inaundwa na Wakuu wa sehemu na vitengo,viongozi wa dini,wazee wa mila,Jeshi la zima moto na uokoaji,Chama cha msalaba mwekundu pamoja na vyama vya siasa.
Mafunzo hayo yanayoendeshwa kwa siku mbili yanatajiwa kwisha siku ya Jumanne tarehe 25 /02/2020 yamedhaminiwa na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania.
(Kwa picha mbalimbali angalia sehemu ya Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.