Mkoa wa Manyara unakwenda kuweka historia ya kuwa mwenyeji wa matukio matatu ya Kitaifa ikiwemo uhitimishaji wa Mbio za Mwenge Uhuru 2023, Ibada maalum ya Kumbukizi ya Kifo cha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa 2023.
Akizungumza na wanahabari mapema leo katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati, Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amesema kuwa mkoa umepata neema ya ajabu kwa kupata matukio makubwa ya kitaifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa katika Ibada iliyofanyika katika Kanisa la Parokia ya Roho Mtakatifu iliyopo katika Mtaa wa Ngarenaro Mjini Babati imesema kuwa ibada hiyo itaanza saa 1.30 asubuhi na itaendeshwa na Mhashamu Baba Askofu Anton Lagwen. Ibada hiyo itahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mama Maria Nyerere pamoja na viongozi mbali mbali watakaokuwa wameambatana nao.
"Niwaombe Wananchi wa Mkoa wa Manyara pamoja na wageni wote kutoka nje ya mkoa wajitokeze kwa wingi, kwanza kumpokea Rais wetu mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wote watakaoambatana nae katika mkoa wetu, vile vile niwaombe mjitokeze kwa wingi siku ya tukio lenyewe Katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa," amesema Mhe. Queen.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.