Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe .Charles Makongoro Nyerere amesema katika Mkoa huu wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wataingia darasani bila usumbufu wowote kwa kuwa Serikali imejenga madarasa ya kutosha.
Makongoro amesema hayo leo Januari 10, 2023 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa Madarasa shule ya Sekondari ya kutwa Magugu na shule mpya ya Sekondari Sarame kata ya Magugu wilaya ya Babati.
Amesema milioni 40 za tozo zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan zimejenga madarasa mawili shule ya Magugu na Milioni 470 zimejenga shule mpya ya Sekondari Sarame kupunguza makali ya wanafunzi kwenda umbali mrefu.
Aidha ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Babati kwa kufanya vizuri katika ujenzi wa Madarasa hayo ya Mama Samia Suluhu Hassan.
RC Makongoro amewataka wazazi wenye watoto wanaopaswa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2023 kuwapelekea shule bila kujali hali walizo nazo kwa kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kila mtoto anapata Elimu.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.