Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan amewataka wazalishaji wa mbolea kuendelea na uzalishaji wa mbolea kwa wingi na kujitahidi kusambaza mbolea hizo kwa wakulima ili kuongeza mazao mashambani
Makamu wa Rais ameyasema hayo akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake alipotembelea kiwanda cha kuzalisha mbolea huko Mnjingu Mkoani Manyara.
Kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bwana Toxic Hans alisema kuwa kiwanda cha Minjingu kimesaidia jamii ya Kijiji cha Minjingu kwa kujenga zahanati,madarasa, na kusaidia mradi wa maji kwa wananchi wa kijiji hicho.
Vilevile Makamu wa Rais aliwataka wazalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho kuacha mara moja kuweka mbolea katika mifuko yenye nembo ya nje ya nchi kwa mbolea hiyo inazalishwa Tanzania. “Nawapongeza kwa juhudi zenu mnazozifanya kuzalisha mbolea kwa wakulima wetu lakini achani tabia ya kuweka mbolea kwenye mifuko yenye nembo ya nje ya Nchi” Mama Samia alisisitiza.
Mara baada ya kutembelea kiwanda hicho Makamu wa Rais alitembelea Ofisi za Mamlaka ya Maji Safi mjini Babati (BAWASSA) na kulizindua rasmi.
Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwapongeza Viongozi kwa ujenzi wa jengo la kisasa na kuwataka BAWASSA kuhakikisha Mamlaka inaongeza mtandao wa maji ili kuwa na wateja wengi na kujiongezea mapato.
Mama Samia pia alitembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara na kuweka jiwe la msingi na kupongeza ujenzi wa Hospitali hiyo unavyotumia gharama ndogo kama fedha zitasimamiwa vizuri.
Baada ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara alitembelea na kuzindua Barabara zinazojengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Babati na kufanya mkutano wa hadhara kwa kuongea na wananchi katika uwanja wa Kwaraa.
Ziara ya Makamu wa Rais itaendelea tena tarehe 18/11/2018 kwa kutembelea Wilaya ya Hanang.
(Kwa picha mbalimbali na Video angalia sehemu ya Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha na Maktaba ya Video)
Imeandikwa Na: Haji A. Msovu
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.