Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeshatoa zaidi ya shilingi 334 bilioni kuboresha miundombinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia Mradi wa Uboreshashi na Uimarishaji Mamlaka za Serikali za Mitaa ( ULGSP).
Hayo yamesenwa na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Barbara Mijini na Vijijini (TARURA) Eng. Victor Seif wakati wa ufunguzi wa kikako cha kazi cha tathimini ya utekelezaji wa mradi wa ULGSP kilichofanyika katika ukumbi wa AICC, Jijini Arusha.
Eng. Seif alieleza kuwa Serikali kupitia Ofisi yaRais Tamisemi imeshatoa idadi hizo za fedha katika Halmashauri 18 zinazotekekeza mradi wa ULGSP zikiwemo; Moshi, Singida, Shinyanga, Geita, Musoma, Bariadi, Bukoba, Songea, Njombe Iringa, Sumbawanga, Mpanda, Tabora, Morogoro, Korogwe, Kibaha, Lindi na Babati, ili kuboresha miundombinu na huduma za kijamii kwa lengo la kupunguza kwa wananchi na kuboresha maisha yao.
“Mradi huu umebadili kabisa sura na madhari ya miji hii inayotekeleza mradi huu kutokana na miundombinu bora iliyojengwa na kuboresha shunguli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi,” alisema Seif.
Alieleza kuwa sasa mradi umefanikiwa; kukamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa 105.8 Km na nyingine 47.1 km zipo kwenye hatua mbalimbali za kukamilishwa,” alisema Seif.
Pia alieleza kuwa kuna mikataba mbalimbali iliyosainiwa ambapo utekelezaji unaendelea ni ujenzi wa Stendi Tisa (9) za mabasi za kisasa ambapo stendi tano zimeshakamilika na zinatumika na Nne (4) zipo katika hatua mbalimbali za kukamilika.
Halikadhalika alieleza kuwa maeneo mengine yanayotekelezwa kupitia fedha hizo ni ujenzi wa machinjio za kisasa Nne (4), masoko ya kisasa mane (4) pamoja na sehemu ya maenesho ya malori (Lorry packing) moja.
Eng. Seif alizitaka Halmashauri zinazotekeleza miradi hiyo kuhakikisha kuwa inatunzwa na kudumu kwa manufaa ya jamii.
“ Ni vema sasa mhakikishe kuwa bajeti ya kutosha inatengwa kwa ajili ya matengenezo na ukarabati na kuzikabidhi barabara zilizokamilika kwa TARURA kwa ajili ya ukarabati kwa wakati (timely maintenance),” alieleza Seif.
Aidha alizitaka Halmashauri kushirikiana na wananchi katika kutunza miundombinu iliyojengwa hasa ya stendi, machinjio na mifereji ya mvua ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Pia Eng. Seif aliwashukuru wadau wa maendeleo hasa Benki ya Dunia kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali mijini hasa za miundombinu kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande wake Kiongozi wa kikundi kazi cha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka Benki ya Dunia bwana Erick Dickson alisema kuwa ni lazima sasa Halmashauri zinazotekeleza miradi hii kuhakikisha kuwa miradi inawanufaisha wananchi na kugusa maisha yao halisi, si kuangalia kilomita ngapi za barabara zimejengwa Peke yake.
“Lengo kubwa la mradi huu si kujenga miundombinu pekee bali ni kubadili maisha ya jamii husika na kuleta manufaa katika maisha yao. Ni lazima sasa muanze kufuatilia na kuchukua taarifa kutoka kwa wananchi wamenufaikaje na miradi hii,”alisema Erick.
Mradi wa ULGSP unatejelezwa katika Halmashauri za Manispaa na Miji 18 kwa fedha za mkopo nafuu takribani USD 255 milioni kutoka Benki ya Dunia kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Chanzo:www.tamisemi.go.tz
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.