Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara imetunukiwa tuzo ya kitaifa ya heshima ya nyota tatu kwa vituo vyake vya afya kumi na mmoja kutoa huduma bora za afya.
Hati hizo zimetolewa siku ya Jumapili na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mh.Dkt.Faustine Ndugulile baada ya kuridhikana utoaji wa huduma hiyo mbele ya Mbunge Mteule wa Simanjiro Bw.James Ole-Milya baada ya kupita bila kupingwa muda mfupi baada ya kutangazwa kwake na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo la Simanjiro.
Kwa maana hiyo Vituo vya Afya vya Orkesumet na Mirerani ndio Vituo vinavyotoa huduma bora kuliko vituo vyote vya Afya Mkoani Manyara.
(Kwa picha mbalimbali na Video angalia sehemu ya Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha na Maktaba ya Video)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.