Napenda kuwafahamisha kuwa terehe 20 Julai 2022 Mkoa wa Manyara utakuwa mwenyeji wa Maadhimisho ya Kitaifa ya siku ya Idadi ya watu Duniani .Maadhimishi hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo “ DUNIA YA WATU BILIONI 8 KUHIMILI WAKATI UJAO NI FURSA YA HAKI KWA WOTE: SHIRIKI SENSA KWA MAENDELEO ENDELEVU”
Maathimisho hayo yatafanyika katika uwanja wa Kateshi “B” Wilayani Hanang ambapo Mgeni rasmi atakua Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa Waziri Mkuu Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ataongozana na ugeni wa viongozi wa Kitaifa na Kimataifa
Ndg Wananchi:
Katika shughuli za utangulizi kabla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya watu Duniani tunakusudia kua na maonyesho ya wafanya biashara na wajasiriamali kwa muda wa siku 3 (kuanzia tarehe 18_20) hivyo wote mnakaribishwa kutangaza kibiashara …
Pia tarehe 19 Julai 2022 katika ukumbi wa White Rose wilayani Babati tutakua na kongamano kubwa la Kitaifa litakalo husisha Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Manyara ambapo mada mbalimbaliu zitazungumzwa ikiwemo:
1… Ujumbe maalumu wa siku ya idadi ya watu duniani
2… Mapambano dhidi ya Ukatili wa Kijinsia na
3… Umuhimu wa Sensa ya watu na Makazi na maandalizi yake kwa ujumla
Hivyo niwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kutoa mawazo na maoni kwenye mada zitakazojadiliwa siku hiyo
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.