Mkuu wa mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti ametoa wito kwa viongozi wa mkoa na wilaya watakaosimamia utekelezaji wa mpango wa usajili wa Watoto walio na umri chini ya miaka mitano mkoani hapa kudumisha uzalendo katika kupata taarifa sahihi za kumbukumbu za kuzaliwa ili serikali iweze kupanga mipango ya mendeleo.
Mkirikiti alitoa wito huo katika semina ya maandalizi ya kuanza utekelezaji wa mpango huo kwa mkoa wa Manyara na Arusha kwa viongozi wa mkoa na wilaya wa mkoa wa Manyara watakaosimamia utekelezaji wa mpango wa huo na kuandaliwa na Wakala wa usajili ufilisi na udhamini (RITA) na kufanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo.
Alisema mipango ya maendeleo ya nchi yoyote hutegemea taarifa sahihi ya ongezeko la watu ambalo litaendana na upangaji wa raslimali fedha na watu katika utekelezaji wake.
Mkirikiti alibainisha kuwa kukosa uzalendo katika upatikanaji wa taarifa sahihi za kuzaliwa kumepelekea baadhi ya wageni kutumia fursa hizo kuajiriwa na kufanya shughuli mbalimbali za ujasiliamali nchini wakidhani kuwa wanahaki hiyo ya msingi
“Tuwe macho na zoezi hili tusikubali kupokea rushwa kwani madhara yake ni makubwa kitaifa na kwamba taarifa sahihi zitoke katika taasisi za kidini na za kisheria kutaepusha maswali na majadil;iano juu ya uhalali wa uraia wa mtu huyo. Alisema Mhe.Mkuu wa Mkoa
Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu,Afisa Mtendaji mkuu RITA Emmy Hudson alisema mpango huo unalengo la kuwajengea uwezo viongozi hao wa kusimamia kikamilifu pindi utakapoanza utekelezaji wake ikiwa ni Pamoja na kuufahamu kwa kina.
Kwa mujibu wake suala la usajili ni jukumu ambalo linamuwezesha mwananchi kuweza kutambulika rasmi katika mifumo ya serikali kwa kuchukua taarifa za mwananchi na kuziingiza katika kumbukumbu za daftari za msajili mkuu wa serikali.
Pia alisema inasaidia kupata takwimu sahihi na kwa wakati kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo ya taifa kwani serikali imekuwa ikichukua jitihada mbalimbali kuweza kuboresha masuala ya usajili nchini ili kupata takwimu sahihi na kwa wakati kuwezesha kupanga mipango ya taifa katika Nyanja za kijamii za afya, elimu na huduma zingine.
Kwa mujibu wa takwimu ya sensa ya mwaka 2012 alisema ilikuwa ni asilimia 13 pekee ya wananchi waliokuwa wamesajiliwa Tanzania nah ii iliifanya Tanzania kuwa ni mojawapo ya nchi ambazo zina kiwango cha chini kabisa cha usajili barani Afrika.
“Serikali imekuja na mkakati wa kitaifa wa kuboresha usajili wa matukio ya binadamu na takwimu (National Strategy on Civil Registration and Vital Statistics) ambao una mipango ya muda mfupi na muda mrefu kwa makundi yatokanayo na umri ili kuifikia ufanisi unaotarajiwa na tayari umetekelezwa katika mikoa 18 ya Tanzania Bara ili kufikia lengo la mikoa 20.” Alisema Emmy.
Alifafanua kuwa utekelezaji wa mpango utarekebisha mfumo wa usajili ambao baadhi ya wazazi na walezi walishindwa kuwasajili Watoto wao ndani ya mud ana kuwapatia vyeti vya kuzaliwa na kwamba serikali imesogeza huduma karibu na makazi wanayoishi katika serikali za mitaa kote nchini katika vituo vya tib ana ofisi za watendaji wa kata.
Aidha alisema kupitia mpango huo serikali imeondoa malipo na ada ya kupata cheti cha kuzaliwa ili Watoto wote bila kujali uwezo wao wa kifedha au mahali wanapoishi ili waweze kuwekwa katika kumbukumbu za daftari la serikali hususani kutoka vijijini.
Mrakibu wa Uhamiaji Dodoma Makao Makuu Grace Rutachokobizwa alitoa Rai kutumia uzalendo katika kusajili kizazi kilichozaliwa ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na sio kwa wageni ambapo kadi za kliniki zilizopatikana katika kupitia daftari la afya, usajili wa wanafunzi mashuleni, viongozi wa dini vikitumika ipasavyo vitasaidia kupata taarifa sahihi.
Alisema umuhimu wa cheti cha kuzaliwa ni utambulisho wa awali kisheria utakaomuwezesha mtoto kupata haki, nafasi za masomo kwa shule za msingi na sekondari na kuzuia ajira kwa Watoto kwa kuwalinda katika masuala ya kisheria.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI Mariam Nkumbwa alibainisha timu za uendeshaji zitasimamia kupata taarifa za kila siku za mwenendo wa usajili wa Watoto kila siku na kuwa ni ajenda ya kudumu katika mikutano yote.
Pia kuwa na ratiba ya kutembelea vituo vyote vya uendeshaji mara kwa mara kujionea mwenendo wa usajili na kubaini mapungufu na kuondoa bakaa ya Watoto chini ya miaka mitano ambao hawajasajiliwa.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.