Vijana Wilayani Kiteto wameishukuru Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Kiteto kwa kuwawezesha kupata mikopo isiyokuwa na riba ili na kuweza kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yamesemwa na vikundi mbalimbali vya Vijana, wanawake na walemavu Wilayani Kiteto mara walipotembelewa na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI walipokuwa wakitembelea na kukagua matumizi ya asilimia kumi na jinsi zinavyogawanywa kwa makundi husika.
Akiongea wakati walipotembelewa na Maafisa hao kutoka TAMISEMI Mwenyekiti wa Kikundi cha Kiteto Vijana Agro Business kinachojihusisha na ulimaji wa mboga na ufugaji wa samaki Bwana Charles Joseph amesema walijiunga vijana hamisini na kuanza kulima bustani na baadae walipewa msaada wa kujengewa Kitalu Nyumba chenye thamani ya Shilingi Milioni Kumi na sita na Ofisi ya waziri Mkuu na baadae kupewa mkopo wa milioni kumi na sita na Halmashauri kupitia asilimia nne za vijana na kujenga kitalu nyumba kinginge kwenye eneo walilopewa na Halmsahuri ya Kiteto na kuanza kulima nyanya.
"Kwa hatua hii tuliyofikia sisi kama vijana tumejipanga kuhakikisha tunafanikiwa kupitia mikopo hii kutoka Halmashauri na tutajitahidi kufanya marejesho kila mwezi ili kuongeza uaminifu kwa viongozi wetu" Alisema Bwa Charles.
Pamoja na vijana hao kuishukuru Serikali kwa mikopo hiyo pia wameelezea changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ikiwemo magonjwa na upatikana wa soko.
Akijibu haja ya changamoto magonjwa Mchumi kutoka TAMISEMI Bwana.Fulgence Matemele aliwata maafisa kilimo kuwatembelea vijana hao mara kwa mara ili kuhakikisha wanapata viwatilifu vya kujinga na mbogamboga hizo ikiwemo kuwatafutia soko la bidhaa zao hata nje ya Kiteto.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Wilaya ya Kiteto Bwana Marsi Kisarika Urassa ambaye anafuga kuku amesema kuwa yeye kama mlemavu anaishukuru sana Halmashauri ya Kiteto kwa mkopo aliyopewa na kuwashauri walemavu wenzake wasibweteke kwa kuwa ni walemavu kwani ulemavu sio sababu ya kutokufanya kazi.
Bwana Urassa ambaye ni mlemavu wa Mguu na mkono kupitia mkopo huo ameweza kufuga kuku zaidi mia moja na kulimiki shamba la ekari kumi.
Akielezea changamoto za walemavu kupata mkopo Halmashauri Bwana Urassa alisema kuwa tatizo kubwa ni kuwa walemavu wanatakiwa kujiunga katika vikundi ili kuanzisha miradi lakini tatizo kubwa ni ulemavu unatofautiana.
"Tunashindwa kujiunga katika vikundi kwa kuwa unaweza kuta kila mtu ana ulemavu tofauti kwa hiyo tunashindwa kuanzisha mradi mmoja, tungeomba serikali iangalie sheria upya ili sisi walemavu tuweze kupewa Mikopo kwa mmoja mmoja" Alisisitiza Bwana Urassa.
Akitoa ufafanuzi kuhusu sheria za walemavu kupewa mikopoa binafsi Afisa rasilimali fedha kutoka TAMISEMI bwana.Ismail Chami amesema kuwa sheria itabadilishwa ili walemavu waweze kukopa mikopo binafsi ili kila mlemavu aanzishe mradi wake kulingana na ulemavu unaomkabili.
Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imeamua kupitia kila Halmashauri nchi nzima kuona jinsi mikopo ya asilimia nne kwa wanawake, asilimia nne kwa vijana na asilimia mbili kwa walemavu inavyotolewa na kuhakikisha mikopo hiyo inatolewa bila ya riba.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.