Kampuni ya Crop Bioscience Solution (T) Ltd imeanza kutoa elimu kwa Wakulima wa Mkoani Manyara jinsi ya kutumia teknolojia katika mfumo wa kifurushi ili kuongeza uzalishaji wa mazao katika mashamba yao.
Akihutubia wakulima katika Kijiji cha Endasago wilayani Babati waliofika kujionea jinsi mfumo huo unavyofanya kazi Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati Bwana Halfani Matipula ameishukuru kampuni ya Crop Bioscience Solution kwa kuwaletea wakulima wa wilaya ya Babati na Mkoa wa Manyara kwa ujumla kwa kuwaletea wakulima wa Manyara teknolojia hiyo na kuwataka wakulima kuungana ili kuitumia kampuni hiyo kulima kisasa ili kujipatia mazao bora na mengi.
“Huduma ya kupanda shamba la mkulima inahitaji kuandaa shamba kwa trekta,mbegu, mbolea na upandaji wa shamba lkn ili mkulima apate teknolojia sahihi kwa wakati na yenye ubora ni vema wadau wote wa kilimo wakaunganishwa katika mfumo wa kifurushi!!” Alisema Bwana Matipula.
Pamoja na kuzindua teknolojia mfumo wa kifurushi kwa wilaya ya Babtai Katibu Tawala Bwana Halfani Matipula pia amewataka wakulima kujiunga Pamoja ili kuweza kupata kupata huduma hiyo kwa unafuu kwani itawarahisishia watoa huduma hiyo kuwafikia wakulima wengi katika eneo moja.
Akiongea wakati wa kumkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Crop Bioscience Solution Ltd Bwana Wilfred Mushobozi amesema kuwa ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wakulima wengi wanashirikiana na Benki ya Dunia kuweka vituo katika mikoa yote ya kanda kanda ya Kaskazini na kwa awamu ya kwanza lengo ni kuwafikia wakulima 5000 lakini kwa msimu huu wa kilimo watawafikia wakulima 2500.
“Mheshimiwa Mgeni Rasmi ili wakulima waendane na hali ya hew ani lazima kutumia zana bora na kwa kuwa tunafahamu wakulima wetu hawawezi kumudu kununua zana bora ndo maana tunawahimiza wajiunge ili tuweze kuwaletea mfumo huu kwao na hatimaye kuongeza uzalishaji katika mashamba yao” Alisema Bwana Mushobozi.
Mkurugenzi Mtendaji huyo Bwana Mushobozi amesema kuwa kwa kutumia Teknolojia ya mfumo wa kifurushi mkulima ataweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo kulimiwa shamba kwa kutumia vifaa bora vya kilimo endelevu kwa gharama nafuu,Vijiji vitapata taarifa ya afya ya udongo,wakulima watapata vifaa vya kupandia kwa wepesi na kwa gharama nafuu, mbolea na mbegu zitamfikia mkulima kwa wakati na bei nafuu na pia wakulima watapewa ushauri kupitia kwa maafisa ugani na mawakala wa teknolojia ya kilimo.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi Afisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bi. Paulina Joseph amewataka wakulima wa Mkoa wa Manyara kuacha kutumia zana duni kama jembe la mkono kwani zana hizo zinafanya kuwa na uzalishaji kupungua kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Mkulima aliyeamua kutumia mfumo huo katika Kijiji hicho bwana Daniel Akonaay amesema kuwa baada kutumia mfumo huo anatarajia kupata mazao mengi kwani mwnzoni alikuwa anakadiria hata ukubwa wa shamba lake kwani mfumo huo umewezesha kupimwa shamba hilo kipimwa kwa kutumia kifaa maalumu cha kupimia (GPS).
Naye Bwana Antony John amewashauri wakulima wenzake kutumia mfumo huo wa kifurushi ili kuhakikisha wanapata mazao bora na mengi.
“Tunamshukuru huyu baba kwa kutuletea mfumo hu una tunaahidi kuwa na sisi tutaanza kulima kwa mfumo huu kwa kweli Bwana Mushobozi ametuletea elimu nzuri sana hapa Kijijini kwetu” Alisema Bwana Antony John.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.