Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Musabila Kusaya amewataka wakulima nchin kutumia mbolea zinazozalishwa nchini Tanzania.
Katibu Mkuu ameyasema hao leo Agusti 28,2020 akiwa katika ziara ya siku moja Mkoani Manyara alipotembelea kiwanda cha kuzalisha mbolea cha Minjingu na kuona ina mbalimbali za mbolea zinazozalishwa katika Kiwanda hicho.
Akiwa kiwandani hapo Katibu Mkuu amevitaka viwanda vya kuzalisha mbolea kuzlisha mbolea bora ili mkulima aweze kupata mazao mengi na bora ili aweze kuinua kipato cha kila siku kwa kulima katika eneo dogo na kupata mazao mengi.
“Tuhakikishe mkulima analimakidogpo na anavuna san ana atumie mbolea bila kulalamika kuwa mbolea aliyoyumia haifai” Alisema Bwana Kusaya.
Katibu Mkuu huyo amesema kuwa kwa wakulima kutumia mbolea zinazozalishwa Tanzania kutasaidia mbolea hizo zipatikane kwa haraka na kwa bei nafuu kwa wakulima, kuonmgeza ajira kwa watanzania na kuongeza pato la Taifa kwa viwanda nchini kulipa kodi kwa nchi.
Kwa upande mwingine Katibu Mkuu huyo amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisaha zinakuwa na Maabara za kupima udongo na pia wataalamu wa kilimo kuwapa ushauri wakulima juu ya mbinu bora za kilimo ili kujikwamua na umasikini.
Kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mkurugenzi wa Kiwanda cha Minjingi Bwana Hans Toxic alisema kuwa kiwanda kina matarajio ya kuzalisha tani 500000 za mbolea ifikapo mwaka 2025 na kumuhakikishia Katibu Mkuu kuwa watajitahidi kuzalisha mbolea bora na kuisambaza katika mikoa yote ya Tanzania.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.