Wanafunzi wawili shule ya sekondari Chief Dodo Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara washinda tuzo kitaifa katika mashindano ya Young Scientist Exhibition yaliyofanyika jijini Dar es saalam mapema mwaka huu. Wanafunzi hao ambao ni Editha Philipo Kidato cha Nne na Nasra mkochi Kidato cha tatu ni mara ya nne kushiriki mashindano hayo walishinda ushindi wa jumla yaani wa kwanza na kuzishinda shule tisini na tano zilizoshiriki katika projekti tisini na tano (95) zilizoshindanishwa.
Awali akizungumzaMkuu wa shule ya sekondari chief Dodo Ndg; Jackson B Warae alisema kuwa wanafunzi hao walishinda katika projekti yao ya mti uitwao Kivumbasi ambao hutumika kuwavutia nyuki kuingia kwenye mzinga katika vipindi vyote vya mwaka hata katika kipindi cha kiangazi,pia alisema wanafunzi hao wanatarijia kushiriki katika mashindao ya kitaifa ya nchi za Afrika yatakayo fanyika mwezi Oktoba mwaka huu nchini Afrika kusini na wataiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia yatakayofanyika mapema mwezi Januari mwakani huko nchini Ireland.
Aidha akitoa wito kwa wanafunzi hao Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mh;Chelestine Mofuga alisema kuwa amefurahishwa na ushindi huo alitoa rai kwa walimu na wanafunzi kuweka kipaumbele katika masomo ya sayansi na hasa watoto wakike kuzidi pewa nafasi pia aliitaka jamii kutojingea mfumo dume kwani hata watoto wakike wanaweza pia alisema wazazi wanapaswa kutoa fursa kwa watoto wote kwa kuwapeleka shule hasa watoto wa kike.
(Kwa picha mbalimbali angalia sehemu ya Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Imeandikwa na: Isabela Joseph (Mafunzo kwa Vitendo UDSM)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.